RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

'NI HALALI WANANCHI KULIPA USHURU WAKATI HAWAPATI HUDUMA?'-MBUNGE HUSSEI...



Headline kutoka bungeni Dodoma June 02 2016 kazi ilikuwa ni maswali na majibu kutoka kwa wabunge kuielekezea Serikali, kazi ya ufafanuzi ilikuwa ikitolewa na Mawaziri. Wabunge mbalimbali waliipata nafasi hiyo ya kuwasilisha maswali yao, lakini hii yaMbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe yeye alisimama kutoa taafifa rasmi.

Hapa anasema…>>’Leo saa tisa usiku katika soko kuu la wilaya ya Nzega kumetokea moto mkubwa ulioteketeza baadhi ya maduka ya wafanya biashara, lakini hoja yangu ni kwamba kwa miaka mitano wamekuwa wakilipa ushuru wa zima moto na taasisi hii imeshindwa kuwapatia huduma wananchi.

‘Sasa nataka tujadili kwa pamoja pale ambapo mwananchi anatimiza wajibu wake wa kidheria wa kulipia huduma kwenye taasisi na taasisi hiyo inashindwa kumpatia mwananchi huduma. Je, ni halali wananchi kuendelea kulipa ushuru wakati hawapewi huduma stahiki‘