RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PAPA FRANCISKO: ZINGATIENI UNABII WA KWELI


Baba Mtakatifu amewataka wakristo kutokuwa na shingo ngumu kwa kufunga mioyo yao juu ua Unabii unaopaswa kuvuka mipaka na kwenda mbali zaidi.

Katika maisha ya kiimani, kuna matumaini lakini pia kuna hatari ya kuweza kuzima amana ya kumbu kumbu na mwendelezo kutoka kwa Roho Mtakatifu.

Mesema huu ndio mwelekeo uliooneshwa na Wakuu wa Makuhani na waandishi kama inavyosimuliwa katika kitabu cha Marko.
Amesema Hawa walitaka kumfunga mdomo Kristo kama ilivyojitokeza kwenye mfano wa vibarua wauaji waliowatesa, wakawapiga kwa mawe watumishi wa Bwana mwenye shamba na hatimaye wakamuua hata Mwanaye wa pekee, ili waweze kurithi shamba lile! Mauaji ya watumishi na Mwana wa pekee ni picha inayotumiwa kwa ajili ya Manabii kwenye Agano la Kale na Yesu kwenye Agano Jipya.

Hawa ni watu waliojifunga katika ubinafsi na undani wao, kiasi hata cha kushindwa kujifunua kwa ahadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu.

Baba Mtakatifu amesema, hawa ni watu wasiokuwa na kumbu kumbu hai wala matumaini.

Wakuu wa Makuhani na waandhishi walitaka kujenga kuta za utengano zinazojikita katika sheria, mfumo wa maisha uliofichika katika ubinafsi.