RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HATIMAYE PAUL CLEMENT AITAMBULISHA UMERUDI NYUMA VIDEO,IANGALIAE HAPA


Jumapili ya leo kupitia kipindi cha Chomoza mwanamuziki wa Injili nchini Paul Clement akiambatana pamoja na meneja wake Gee maarufu, mmoja wa maproducer wake John Marco na Jesca Honore wameitambulisha rasmi video yao iitwayo Umerudi Nyuma.Video hii iliyokuwa ikisubiriwa kwa takribani wiki kadhaa imeonyeshwa live kwenye kipindi hicho kutoka Clouds Tv kinachoongozwa na Jimmy Temu pamoja na Samuel Sasali.Video hiyo mpya imefanywa chini ya Fishers Video production na imekuwa directed na EINXER ambaye kwa sasa anafanya vizuri sana nchini huku audio ikiwa imefanywa na Fishers records pamoja na Innocent Mujwahuki(Kanye).


Akiitambulisha nyimbo hiyo Gee Maarufu amesema nyimbo hiyo imewaweka bize kwa muda mrefu lakini hatimaye imetoka.Samuel Sasali kwa upande wake amesema video hiyo imeonyesha ubora kuanzia kwenye audio Production,rangi ya video, script yake ambayo ndani yake inaionyesha familia moja ambapo mama wa familia anaonekana akimlaumu mumewe kuwa amerudi nyuma kwa kumuhusisha na mahusiano nje ya ndoa yao.Kwa mujibu wa Paul na Gee nyimbo hii itaanza kuonekana kwenye Youtube musda wowotena itapatikana kwenye mtandao wa Mkito.