RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

PICHA 22: DUBAI INAONGOZA LIST YAKUWA NA MAJENGO YALIOVUNJA REKODI KWA UREFU DUNIANI

Mtu wangu usisahau kuwa Ukuaji wa Miji mikubwa ndio matokeo mazuri ya teknolojia inayosababisha kuwa na miundombinu bora. June 20 2016 nakusogezea picha 22 za majengo yaliyochukua headlines kwa urefu zaidi duniani kutoka kwenye nchi tofauti.

Dubai ikiwa kama nchi inayoongoza kwa kuwa na majengo mengi yalioenda hewani, nchi zingine kama Tokyo, Japan, Marekani, Saud Arabia na Malaysia pia usisahau kuniachia comment yako hapo chini mtu wangu.

Jengo hili litajengwa nchini Dubai na kuzinduliwa 2020 lina urefu wa futi 3044 kwenda hewani.



Jengo la Burj Khalifa lililopo nchini Dubai lenye urefu wa futi 2717 kwenda hewani.

Jengo hili la Jedah Tower lililopo nchini Saudi Arabia na bado lipo katika ujenzi lenye urefu wa futi 3280 kwenda juu.


Jengo hili la Sky mile Tower lililokamilika kujengwa na kuzinduliwa Feb 2016 lililopo nchini Tokyo lenye urefu wa futi 5250 kwenda juu.



Jengo hili la 1 undershaft lililopo London nchini Uingereza lililozinduliwa December 2015 lenye urefu wa futi 984 kwenda juu.



Jengo hili la Shaghai Tower lililopo nchini China lililozinduiwa 2015 nakutajwa kuwa jengo refu kuliko yote kwa bara la Asia lenye urefu wa futi 2073 kwenda juu.




Jengo hili la Mecca Royal Clock Tower Hotel lililopo nchini Saudi Arabia karibu na Msikiti mtakatifu wa Maka lenye urefu wa futi 1972.


Jengo hili la One World Trade Center lililopo nchini Marekani na limetajwa kama jengo refu kuliko yote kwa upande wa mabara yaliopo magharibi mwa dunia lenye urefu wa futi 1779 lenye floor 94.



Jengo hili la Taipei 101 lililopo nchini Taiwan lenye urefu wa futi 1667 na lina floo 101.


Jengo hili la Shaghai World finacial Center lililopo mjini Shaghai nchini China lenye urefu wa futi 1614.17 lililojengwa kwa mda wa miaka 11 na kuzinduliwa rasmi 2008.




Jengo hili la International Commercial Center lililopo Hong Kong nchini China lenye urefu wa futi 1588 na floo 108 kwenda juu.



Jengo hili la Petronas 1 and 2 lililopo Kuala Lumpur nchini Malaysia limetajwa kua jengo refu ambalo ni pacha duniani lenye urefu wa futi 1483 na floo 88.