Bwana Yesu apewe sifa watu wa Mungu. Kwa jina naitwa Andrew Kiwhelo mwimbaji wa
nyimbo za Injili Tanzania na mzaliwa wa Iringa ila naishi jijini dar es Salaam,
nimeoa mke mzuri na mpenda kutoka nchini Kenya. Leo hii nipo mahali hapa
kuelezea jinsi navyoifahamu redio ya Praise Power 99.3FM ambayo iko chini ya
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” jijini
Dar esa salaam Tanzania.
Mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania, Andrew Kiwhelo (kushoto) na mtangazaji wa Praise Power Radio 99.3FM Ben Bonge na Rumafrica Lets Talk katika studio ya Rumafrica
Binafsi nimeifahamu Praise Power Radio kipindi nipo kwenye bendi moja ya muziki
ambayo siwezi kutaja jina kwa sasa. Nakumbuka siku moja katika harakati zetu za
kutaka kuzitangaza nyimbo zetu redio, tuliamua kukaa chini na waimbaji wenzangu
na kuamua kupeleka nyimbo zetu Praise Power Radio ili zipigwe na kusikika na
watu wengina nah ii ilikuwa ni mwaka
2004 au 2005
Praise Power Radio imefanyika faraja kubwa sana katika maisha yangu na pia kwa
Watanzania walio wengi. Mimi kipindi hicho cha nyuma nilikuwa mshiriki wa
kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” na nimeona uzuri wa hii redio.
Nimebahatika kusikiliza redio nyingi sana hapa Tanzania lakini Praise Power
Radio imekuwa faraja sana kwangu ukifananisha na redio zingine. Redio hii
imekuwa haibagui aina ya watumishi wa Mungu. Kwetu sisi waimbaji tumekuwa
tukipata ushauri kutoka kwa watangazaji tunapopeleka nyimbo zetu redio, na pale
ambapo kuna upungufu wamekuwa wakitushauri cha kufanya ili kuboresha huduma
yetu ya uimbaji.
Tunamuomba sana Mungu azidi kumbariki sana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa
maono ya kuanzisha kituo hiki cha redio. Kupitia redio hii mimi nimeweza
kufahamika na watu wengi sana kuanzia ile albamu yangu ya kwanza na ile ya
pili, hakika wameweza kusimama na mimi tangia kipindi hicho cha nyuma mpaka leo
hii. Praise Power redio imenisaidia sana kwa mambo mengi mno ambayo mengine
siwezi hata kuyataja.
Ningependa kushauri kwa yeyote ambaye amewahi kusikiliza Praise Power Radio
99.3FM na Yule ambayo nib ado wajitahidi sana kuendelea kusikiliza redio hii
kwa kuna vipindi vya kukuelimisha kutoka kwa watangazaji ambayo wamejitoa
kufanya kazi ya BWANA na wamejipanga vizuri pia wanajituma kumtumikia Mungu kwa
unyeyekevu sana.
Mimi binafsi ninapenda sana vipindi vya Praise Power Radio 99.3FM hasa kipindi
cha Rise and Shine chini ya Veronica Frank, Kesha na Praise Power chini ya
Erick Brighton na John Kissaka, Sifa Moto chini ya Bony Magupa, Jamvi Chini ya
Ben Bonge, Joyce na Frida, pia kipindi cha Power Drive ambacho huzungumzia nchi
yetu ya Tanzania kwa undani zaidi, Faraja Time chini ya Victor Aron
Kuna watu wengi sana wanabarikiwa
sana na vipindi vya Praise Power Radio, watu wanapokea miujiza yao na uponyaji
wanaposikiliza watangazaji na watumishi wa Mungu wanahubiri kupitia redio hii
Watangazaji wamejipanga vizuri na katika mazungumzo yao wanatoa maneno ya
faraja kutoka kwenye Biblia. Radio ya Praise Power haichagui rangi, kabila,
taifa wala jinsia, ni radio ya watu wote.
Mwisho nataka kuwajulisha kuwa nyimbo zangu unaweza kusikia katika redio hii ya
Praise Power Radio 99.3FM na albam yangu mpya ya BUSH TO TOWN inapatikana
sokoni kwa sasa. Kwahiyo ukitaka kusikiliza nyimbo zangu kama vile ONEKANA LEO
na nyingine nyingi usikose kusikiliza hii redio ambayo ni mkombozi wetu katika
kutangaza kazi na huduma zetu.
Ukitaka kunipata mimi na ukatamani kunialika kwenye mkutano, semina, kongamano
au tukio lolote la kumtukuza Mungu basi wasiliana name kwa simu hizi, o716 470
104 au 0763 416 382, Mungu akubariki sana na endele kusoma Gazeti Rumafrica
Online Magazine, Kusilikiza Praise Power Radio na kuangalia Rumafrica Online TV
pamoja na Mlima wa Moto TV. Nakupenda