RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DANSTAN MABOYA ALIVYOUNGURUMISHA KATIKA SEMINA YA CROSSOVER MLIMA WA MOTO MIKOCHENI |B| SIKU YA JUMAPILI 03/07/2016

Bwana asifiwe sana, ninaomba umsalimie rafiki yako na umwambie upo mahali sahihi. Sasa ninaomba umpe Roho Mtakatifu dakika 30. Ninashkuru Mungu kwa neema ambayo inazidi kuzidi siku hadi siku, na neema hiyo ikaendelea katika kujenga mwili wa Kristo.

Nilikuwa nikiguswa sana na ushuhuda wa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliokuwa unahusu miogo aliyokuwa anategemea, halafu mtu akaweka mafuta ya taa badala ya maji. Sasa haya tunaita “maudhi”, Ni sawasawa na siku umeamua kuingia kwenye zamu yako, na unajiandaa jioni ili upate kitu ulichokitega kukilamba na saumu ilikuwa hatari sana halafu unakuta hakipo, hayo tunaita “maudhi”. 
 Maudhi kama hayo mara nyingi huwa yanatokea, na Mungu anasema, “Waombeeni adui zenu na wabarikini wanaowaudhi” Umetoa suruali yako wakupigie pasi, ghafla imeungua, hayo tunasema ni “Maudhi”. Unaweza kufanya vitu vingine vya maudhi vikakupeleka “Central Police”. Na ndio maana Mungu ametupa busara ya kutokuwa na tabia ya kushikilia maudhi. 
Ninamshukuru Mungu katika mtiririko wa wiki nzima wa kufanya semina ya Mid- Crossover hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”, Mungu alinipa neema ya kuzungumzia baadhi ya mambo, na baadhi ya hayo ni kondoo husikia sauti ya mchungaji, Mungu kuhusika kuijenga madhabahu ya Mlima wa Moto na Watu kufungua fikra zao.


KONDOO HUSIKIA SAUTI YA MCHUNGAJI.
Katika dunia hii tunayoishi watumishi wapo kumi elfu lakini wanaotuchunga ni wazazi wetu. Kondoo hatakiwi kusikia sauti ya nabii ila kondoo anatakiwa amwambie nabii lakini asimsikilize. Kwa mfano kuna nabii na Mchungaji, Nabii atakaposimama nitamheshimu kwasababu anasimama kwa niaba ya Askofu wangu lakini sauti nitaisikia kutoka kwa mchungaji. 
Kwasababu huko ndiko Napata “balance” na afya. Mchungaji hatakuja kuzungumza kitu chenye mchanganyo, lakini Nabii anaweza kuwa “Comfused” akaweka uongo ndani kwenye huduma yake ili umkubali. Na tunayo mifano mingi kabisa, Geasi alikuwa mmoja wa manabii, alipomuona kiongozi wake akakataa kuchukua ile zawadi iliyotoka kwa Namani. 
Hivyo “prophet” anaweza akawachanganya akili, lakini mchungaji hawezi kwa maana upo naye siku zote kanisani na katika mihangaiko yako unamshirikisha, kwahiyo Nabii anaweza akakubamiza mwanangu.

Mchungaji hawezi kukubamiza kwasababu akikubamiza utamuuliza kwakuwa uko naye siku zote. Mchungaji akikuambia unatakiwa kuleta kiasi fulani cha fedha na utapokea muujiza fulani, sasa ukiona muujiza haujatokea si utamfuata? Lakini Nabii hutaweza kumpata kwasababu atakuwa ameshaondoka na yuko mbali na wewe.

Kwahiyo katika jambo lolote unaloona Mungu amesema nilitende na ni jambo la Kimungu basi mshilikishe mkufunzi wako na utakuwa kwenye hali ya usalama.

Wapo watu wengi sana leo wanawadanganya watu kwa maneno laini kwa waokovu waliowanyenyekevu wanatumbukia kwenye mtego

Ukiona Nabii anasema, “Utakufa” wewe mwambie, “Sitakufa bali nitaishi”, kwasababu huyo ni nabii wa khukumu. Unauwezo wa kuishi, hata kama ni Mungu mwenyewe na umesikia sauti yake inakuambia, “Mwanangu unakwenda kufa leo”, unauwezo wa kupinga kwasababu ni Baba yako huyo. Ezekia aliambiwa, “Utakufa” akagoma na akaongezewa miaka 15 ya kuishi. 
Watu hawaelewi, “Constitution” ya kimbingu. Ezekia alikataa, aliambiwa, “Ugonjwa huu hutapona utakwenda kufa, tengeneza mambo ya nyumba yako kama miradhi na kila kitu” akagoma, akageukia ukutani akamkumbusha Mungu, na Mungu akaona kuna uhalali akamuongezea miaka 15. 
Lakini kuna kuhani mmoja Eli alipewa ujumbe, “ Weka nyumba sawasawa umetenda dhambi, nitakuppiga”, alivyo mjinga akainua mikono yake juu akasema, “Acha Neno la Bwana litimie”, na Mungu akamuondoa yeye na watoto wake siku moja, lakini Ezekia alipona. Ninachotaka kukuambia ni kwamba usijaribu kuweka unyenyekevu badia. Nikuulize, lee hii ukiambiwa, “Utakufa, utagoma au utakubali?” Unataka kufa na hao watoto walioko kwenye nyumba ya kupanga nani awajengee nyumba?

Hata leo hii kanisa lipo kwenye matatizo mengi kwasababu wameshindwa kuheshimu sauti ya mchungaji. Na hii ni “Biblical” ya kwamba kondoo husikiliza sauti ya mchungaji. Na kila mchungaji amepewa “Vision” yake, utakuta kila mtu amepewa maono tofauti na ya mwenzake. Na wewe upo katika kanisa la Mlima wa Moto kwasababu una maono ambayo Mungu amempa mama Gertrude Rwakatare. Ukijikita katika maono ya mchungaji wako ndipo unapata “blessing” ya ujumla.

Kumbuka Mungu ameweka wachungaji, wainjilisti, Manabii, Mitume ambao wapo kwaajili yako, Nakumbuka kuna watumishi wengine ambao walipambana na Paulo sana, kwasababu kuna wengine walikuwa wanahubiri kwaajili ya wito mkuu na wengine kwaajili ya matumbo yao na wengine kwaajili ya mashindano. Tunaweza kuwatambua manabii hao kwa matunda yao.

Watumishi wengi sana hawataki kukaa sehemu moja, na ukiona kuna mtumishi anaweka kitu kilichosimama basi ujue huyo yuko “serious”. Lakini ukiona mtumishi ameweka hem la kufanyia ibada ujue huyo anahama muda wowote, utalifuata hema leo, na kesho halipo.

Unajua safari ya kwenda mbinguni sio ya miezi miwili tu kwani kuishi kwako duniani yawezekana ukaishi mika 40 na wengine miaka 90, kwahiyo unasafari ya miaka 50 ya kwenda mbinguni. Yesu anaposema, Kondoo husikia sauti ya mchungaji humo mna kila kitu. 

Kwahiyo mchungaji wako anakuwa utendaji wake kutoka mbinguni ambapo Roho Mtakatifu anashuka kutoka mbinguni na anakaa ndani yake. Mchungaji wako hawezi kila siku akawa anahubiri “Deliverance” tu, kwani kuna masomo zaidi ya “Deliverance”.

Sasa baada ya kuombewa na pepo kuondoka unatakiwa kufundishwa Neno na Ujasiriamali. Sasa wengine wanataka kila siku kelele, leo niombee kichwa, kesho mgongo, kesho kutwa kiuno. Watumishi wengine wanaanza kutunga na kusema kuna maombi ya kuongezewa afya, nasema, “Huo ni mchicha mwanangu”.

Mungu alitoa vyakula vya bondeni ili uweze kula. Sasa umeamua kujiumiza kwa kula mlo wa aina moja. Na ndio maana mama Gertrude Rwakatare anasema, “Yeye chakula chake, anapiga “Keyboard”.

Mungu anaposema nitaurejesha ujana wako kama tai, ana maanisha atavirejesha vitu vyote vitakavyorutubisha mwili wako, yaani kwenye mwili wako hautapungukiwa na “glucose”, kwasababu chochote utakachokihitaji utakipa. Na chakula ni ibada kamili.

Na chochote kinachofunguliwa na maombi lazima ukiheshimu, na Yesu alisema, “Kabla hujala sali kwanza”. Popote panapofunguliwa na maombi ni lazima uheshimu kwasababu kula ni kalama kutoka kwa Mungu, ila tu usiwe mlafi. Inatakiwa mtu aone meza ya chakula imejaa vyakula, na hapo aseme, “Nafsi yangu, mimi ni Bwana”.

Miezi sita iliyobaki Bwana akutendee mema, kwani mayai, nyama ya kuchoma, “juice” ya machungwa na kila kitu ni halali yako nah ii ni “Gift from God”. Soma Mhubiri 2:24, “Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake”. Kazi zote tunazofanya mwisho wake unaishia kula. 

Ukisoma Mhubiri 3:12, “Mimi ninajua kwamba hakuna jema kwao kupita kufurahi na kufanya mema maadam anaishi., tena ni karama ya Mungu kila mtu apate kula na kunywa na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote” Sasa ninataka ni nani ana karama hiyo ya kupiga “Keyboard” ya mboga mboga kama anavyofanya mtumishi wa Mungu mama Gertrude Rwakatare. Sanasana umewaza wiki hii ninapiga uduvi na minafu. Mwambie rafiki yako kuwa mnafu utakula kwa hamu, na uduvi nitaweka pembeni lakini kuna mzigo wa msosi wa nguvu upo katikati ya sahani.

Chochote kinachofunguliwa kwa ibada lazima kiheshimiwe kwa maana mbingu imehusika. Kuna watu wengine wajanja sana unaweza kuleta ugali na maharage mezani, anaanza kuomba wakati hataki kula ugali maharage ila anatamani wali nyama. Sasa wewe kama hutaki hicho chakula kwanini unaomba Mungu akibariki? Umeenda nyumba ya mtu amekupikia hicho chakula ndicho kilichopo. Unakula kidogo na unakunywa maji mengi, wewe ukiona chakula hukitaka usifanye maombi, kula bila kuomba.

Ninachotaka kusema ni kwamba, “Mungu akishuka anahusika”. Bwana akakutie nguvu, Bwana akabadilishe mambo yako yote. Tunayotaka kuona maendeleo kwa mkristo ni pale tunapomuona alikuwa na pepo akaombewa na akapona na baada ya hapo tunamuona kwenye, “Bible Study”, baadaee anakuwa mama nitile, baadae anauza duka, baadae anajenga, baadae anasafiri mbali; hapo tunasema mtu huyu ni mtu mwenye afya. Sio unaokoka miaka 10 wewe unauza vitabu tu, “No” lazima upande juu. Na mimi kama mtumishi mama Gertrude Rwakatare alivyosema ninakuambukiza usije ukala mihogo ya mafuta ya taa tena, pokeeeeea kwa Jina la Yesu Kristo.


Watu wengine wamechukua tafsiri za Biblia vibaya, wanasema, “Ukiwa tajiri hautaridhi ufamlme wa mbinguni”. Wewe ukipenda fedha hapo ni tatizo, ila ukitawala pesa hapo hakuna tatizo, yaani unakuwa na pesa na ile pesa ukiitawala unakuwa kwenye mikono salama. Na dalili ya pesa inaanzia kwenye hizi pesa ndogo ndogo. Ukiona baba kwenye nyumba akiombwa pesa anageuka nyuma na kuchungulia pesa watu wasijue hapo ujue baba ni tatizo, hana pesa. Hii pesa ya kujikunja kuitoa mfukoni ina nini hii?

Ni lazima upokee mkombozi wa fikra. Mungu anapenda kukuona milionea. Ukiona wewe unakuwa bahari kwa pesa ndogo, Mungu atakosa kukuamini kukupa pesa nyingi. Mimi ninajua katika hii miezi sita kama mtumishi wa Mungu mama Gertrude Rwakatare alivyoomba, kuna jambo kubwa linakwenda kutokea, ninasema, “Pokeeeaaaa”. Si unajua kondoo husikia sauti ya mchungaji na kila aliyesikia sauti ya mchungaji afya hutokea.

MUNGU ALIHUSIKA KUWEKA MADHABAHU YA MLIMA WA MOTO.
Na mtu aliyetukana madhabahu hii anatukana aliyehusika. Kwababu Mungu huwa anaweka kituo kila sehemu kwa aina yake. Yesu alisema hao ulionipa uwe umoja kama sisi tulivyo na umoja ili watu waweze kuona utukufu wako. Ndani ya umoja kuna utukufu. Hata kama tukiomba hapa kwa pamoja atupe ishara na ufufuo wa maiti. Maiti haiwezi kufufuka kama hatutakuwa na umoja.

Kuna magonjwa mengine huhitaji kuwekewa mikono na mtu, unahitaji kuiheshimu madhabahu. Kwamfano mtumishi wa Mungu Mch. Lukumay anatatizo la figo nap engine akaenda Kunduchi kwenye mkutano akapate uponyaji. Na akaitwa na mtumishi akamuombea na akapona, na alipoulizwa anasema mimi ni Mchungaji kutoka katika kanisa la Mlima wa Moto. Je, hapo amekuangusha au amekuinua katika kanisa lako la Mlima wa Moto? Mch. Noah Lukumay anahitaji kupata ule uponyaji wa ki-“VIP” kwasababu kuna kitu ndani yake kinaitwa, “Slighted Fear”, anatakiwa aiamini madhabahu kuwa itampa majibu yote. Na imani huja kwa kusikia na kusikia huja kwa Neno la Kristo.

Unapokuwa umebanwa na homa na ukaenda kuombewa siku nyingine hii inamaanisha wewe unalitukanisha kanisa, kwasababu Mch. Noah Lukumay alishavuka kwenye kuwekewa mikono, ila yeye anatakiwa kupokea ule uponyaji wa ki-VIP”

Nakumbuka kipindi cha nyuma wakati wa vita vya Uganda nikiwa Kariakoo nilibanwa na malaria, nikaamua kujipanga foleni katika hospitali ya Mnanzi Mmoja. Mara akapita mhubiri anayenifahamu akaniuliza, “Heee!! Mtumishi upo hapa?”, nikamwambia, “Ninamsindikiza huyu niliyekaa naye”, Mtumishi Yule hakuamini kuona mchungaji ninayehubiri uponyaji kanisani leo hii nipo hospitalini kupata matibabu, na alipotoka nikaingia hospitalini, nikatokea mlango wa pili, mbiooo. Nikafika sehemu nikasema, “Mungu vidonge ninavihitaji, maumivu ni makali na watu hawaniamini kuona mtumishi nipo hapa hospitalini, nifanyaje?” Ndipo Mungu akanipa siri kuwa kuna uponyaji wa watumishi tunaita uponyaji wa ma-”VIP”, na kuna uponyaji wa watu wa kuja au wa kawaida.

Sasa usipoheshimu “title” uliyonayo na usiruhusu kila mtu kila mtu akuwekee mikono kichwani ili akuombee, kwasababu kwa kufanya hivyo kunakuwa na “Transfer” ya “anointing” . Mwingine ana madudu yake na akikubandika unaondoka nayo. Kama Askofu wako mama Gertrude Rwakatare alikubandika ile “anointing” inaendelea.. Na kama mtu ana nguvu zake ashike bega na sio kichwa kwani akishika kichwa utachanganyikiwa. Na hii ni kwasbabu ya kutoelewa.Lengo la Mungu ni kuweka kitu kikae sawa.



Watu watakuja na maneno mengi laini na maneno ya hali ya juu. Kuna watumishi wale wajanja wajanja wanapofika kwenye mji au kanisa wakiwa hawana meseji ya kuhubiri. Huwa wanapenda kuchukua mikanda ya wahubiri wenye majina mjini, wanaisikiliza kwa makini na wanaangalia pale ambapo watumishi hawajahubiri wanaongeza ya kwao. Sasa wakiingia kanisa la mtu kuhubiri, basi waamini wanajua huyu mtumishi ana hekima kweli. Sasa unaweza kuona ya kwamba mahubiri yao yalikuwa ni ya nguvu lakini tabia yao mbaya.

Yesu alisema mtawatambua watumishi wake kwa matunda yao. Hata aje mtu akakuletea neno na likakuvuruga kabisa, kimbilia kwa mchungaji mwambie, “Nimevurugwa”

Kuujenga ufalme wa Mungu sio kuchota kutoka kwenye kapu hili na kupeleka kwenye kapu hili, hiyo inaitwa, “The shifting kingdom” yaani kuhamisha ufalme. Kujenga ufalme ni mimi niwaimarishe ninyi waamini, na ninakwenda mwenyewe kama ni kawe au wapi, ninaanza moja, na sio kuchota hapa kuhamisha pale, hiyo ni kuhamisha ufalme. Na sisi hatujaitwa kuhamisha ufalme badi kujenga ufalme. Na hii imesababisha watumishi wengi kuwa na tabia mbaya, lakini wakiombea pepo linatoka. Sasa kwasababu wewe ulikuwa unaumwa na pepo limetoka unaanza kusema huyu ni bora kuliko mchungaji wako, na hapo unakuwa umetia nguvu katika mikono ya adui muovu na atashughulika na wewe.





Sasa utakuta mtu mzima mwenye miaka yake 50 amekutana na mtumishi mwenye tabia mbaya yatakayomkuta au atakayoyasikia yanabaki moyoni mwake na hawezi kusema kwasababu umri wake hauruhusu kuzungumza. Na mtu huyo ukimwambia twende tena kwa mchungaji aliyeumizwa naye anasema, “Achana naye, kwani hilo ni pepo”. Wenye ubavu wa kuzungumza ni hawa mabinti ma-“teanager” utakuta wanasema, “Yule mhubiri nilimtolea nje, nilifika pale anasema anishike kifua, matiti, Yule ni pepo”. Lakini mama mzima hazungumzi kwasababu anaogopa kuvuruga nyumba yake.

Nilikuwa na rafiki yangu ambaye ni mchungajim mkubwa sana Nairobi, alikaribisha mgeni mmoja kutoka sehemu Fulani, Yule jamaa alipiga injili vizuri sana. Halafu baadae akawa anawaita watu kwenye “hotel” aliyofikia, na wakifika hapo anaanza kuwapa viwango vya pesa vya kumpa ili wapone na majaribu yao. Alikuja mtu mmoja anaumwa figo akamuombea na alipopona akaambiwa apelike 1,000,000 ya Kenya, nay eye alipeleka lakini aliporudi tu nyumbani hali yake ikarudi tena kama mwanzo. Kukawa na vurugu katika familia, na ile familia haikumfuata Yule jamaa bali ilimfuata Yule mchungaji aliyemleta Yule jamaa. Ilikuwa ni kesi kubwa sana, wale ndugu wanataka pesa yao na Yule jamaa amekimbia. Ikabidi mchungaji achukue kiasi cha fedjha katika mfuko wa kanisa ku-“cover” lile deni.
KIPINDI CHA MAOMBEZI, UPONUAJI NA MATENSO MAKUU YA MUNGU

apona kanza ya mapafu













 Apona tatizo la kiuno na nyonga

















 Apona uvimbe katika titi