RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

CARISSA SHARON OYAKHILOME, MTOTO WA PASTOR CHRISS MWENYE KIPAJI CHA UIMBAJI,ANGALIA VIDEO ZAKE.


Carissa Sharon Oyakhilome ni mtoto wa Kwanza wa Pastor Chriss Oyakhilome kutoka katika ndoa yake na Anita Oyakhilome iliyojaliwa kupata watoto wawili wa kike, Mdogo wake na Carissa anaitwa Charlene na kwa pamoja wawili hao wamekuwa wakiishi nchini Uingereza kwa kipindi kirefu sasa huku baba yao akiwa nchini Afrika ya Kusini akiongoza kanisa kubwa duniani liitwalo Christ Embassy.

Carissa Sharon Oyakhilome ama CSO kwa sasa ana umri wa miaka 24 na amekuwa akiimba Gospel kwa muda mrefu.Kwa mara ya kwanza aliachia Video yake iitwayo I’m Excellent mnamo mwaka 2013 iliyofanya vyema sana.Kwa kipindi cha miezi miwili tu toka iachiwe nyimbo hiyo ndani ya Itunes ilikuwa namba 7, katika nyimbo hiyo CSO alimshirikisha Icey Stanley aliyekuwa mpiga Keyboard wa Christ Embasy nchini Africa ya Kusini.


Mwaka 2015 Carissa aliachia video ya nyimbo yake mpya iliyoitwa I do for you iliyokuwa na Swagg nyingi na kuleta maswali kadhaa kwa baadhi ya watu.Tofauti na matazamio ya wengi kwamba binti huyu angejikita vilivyo kwenye uimbaji Carissa amekuwa hatoi nyimbo mara kwa mara kitu ambacho mashabiki wanakilalamikia.Kwa sasa Carissa anajipanga kuachia muvie yake na soon Hosanna Kwanza itakupa more details juu ya Muvie hiyo