RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HARUFU YA KUKU INAZUIA MALARIA - UTAFITI.



Je unaogopa kuambukizwa na ugonjwa wa malaria?

Ikiwa jibu lako ni ndio basi nakupa ushauri nasaha, Fuga kuku!

Utafiti umebaini kuwa ,harufu ya kuku inaweza kukulinda dhidi ya maambukizi ya malaria.

Watafiti nchini Ethiopia na Sweden wamegundua kuwa mbu wanaobeba virusi visababishavyo ugonjwa wa Malaria huwa wanafanya kila wawezalo kukaa mbali na ndege huyo anayefugwa majumbani.


Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Malaria umebaini kuwa mbu hunusa harfu ya mnyama kabla ya kumuuma. Hata hivyo hawajui nini katika harufu ya kuku inawapa kinyaa mbu.

Katika hatua ya pili ya utafiti huo sasa, watafiti hao wanalenga viungo vya harufu ya kuku ilikuunda kinga dhabiti dhidi ya mbu hao wanaoambukiza malaria.

Habtie Tekie kutoka chuo kikuu cha Addis Ababa Ethiopia anasema kuwa mipango inaendelea na huenda majaribio yakatekelezwa karibuni.