MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HATIMAYE MRITHI WA DAVID CAMERON APATIKANA

Mwanamama Theresa May amekuwa mgombea pekee ndani ya chama tawala cha Conservative nchini Uingereza, aliyebakia katika kinyanganyiro cha kumrithi waziri mkuu aliyejiuzulu David Cameron. Baada ya mpinzani wake wa karibu mwanamama Andrea Leadsom kutangaza kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho.

Leo jioni viongozi waandamizi wa juu ndani ya Chama cha Conservative watakutana kumuidhinisha Theresa May kuwa kiongozi mkuu wa chama. Hata kama hataonana na malkia wa Uingereza leo Theresa May atatangazwa kuwa waziri mkuu muda mchache kuanzia leo baada ya kuidhinishwa na chama chake.