RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HITIMISHO LA SEMINA YA MI-CROSSOVER LAFANA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI 03.06.2016


Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya hitimisho la Semina kubwa ya Mid-Crossover siku ya Jumapili 03.07.2016 iliyokuwa ikifanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kuanzia Jumapili 26.06.2016 hadi Jumapili 03.07.2016 aliweza kuwahimiza waamini wa kanisa hilo kufanya maombezi ya kuliombea Taifa la Tanzania na viongozi wake. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Pia waliweza kuimba wimbo wa Taifa na wimbo wa Tanzania. Siku hii ya hitimisho ilihudhuriwa na viongozi wa serikali kama vile Mbunge wa Mbeya Viti Maalum kupitia CCM Mh. Marry Mwanjelwa pamoja na viongozi wa dini kama vile Mch. Sylvanus Komba kutoka Dodoma, Askofu Danstan Maboya kutoka Arusha, Mch. Noah Lukumay kutoka DSM na Mch. Francis Machichi kutoka DSM na wengine wengi. 
Waandishi wa habari nao waliweza kufika ili kupata habari kutokana na uzito wa semina hii. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alikuwa haya ya kusema, “Tumepata neema ya kufikia miezi sita tangia mwaka 2016 uanze na sasa tumepata nafasi ya kukabidhi Mungu wetu miezi sita iliyo mbele yetu yaani kuanzia Julai 2016. 
 Mpaka mwezi Desemba Tutasoma katika kitabu cha Timotheo 2:1-3. Neno la Mungu linasema, Basi kabla ya mambo yote dua na sala na maombezi na shukrani zifanyike kwa watu wote. Kwahiyo Wafalme na wote wenye mamlaka tuishi maisha ya utulivu na amani katika utahuwa wote na ustahimu. Hili ni zuri nalo lakubarika mbele za Mungu mwokozi wetu ambaye hutaka watu wote waokolewe na kupata kujua yaliyokweli. Na hili ndilo Neno la Mungu.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kufungua ibada ya hitimisho la semina ya Mid-Crrossover katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa maombi, na hivi ndivyo alivyoaanza, Sasa ninaomba tuombe, “Baba katika jina la Yesu Kristo, tupo mbele yako pamoja na kanisa la Mlima wa Moto, tukiungana na na watu wote, wachungaji wa kanisani, wazee wa kanisa na wageni wetu waliofika kuabudu nasi tukimuombea Rais wetu, tukiombea Bunge letu na viongozi wote. Baba nimeomba kwa jina la Baba na la Mwana na Roto Mtakatifu nimeomba, na wote tuseme..Amen