RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MAEFU WAINGIA KATIKA KISIMA CHA BETSAIDA WAKATI WA HITIMISHO LA SEMINA YA MI-CROSSOVER MLIMA WA MOTO MIKOCHENI SIKU YA JUMAPILI 03.07.2016:




Siku ya Jumapili 03,07.2016 katika hitimisho la semina Mid-Crossover iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B", baada ya kupokea Neno kutoka kwa watumishi wa Mungu Bishop Dr. Gertrude Rwakatare, Mch. Noah Lukumay, Bishop Dastan Maboya (arusha), Mch. Sylvanus Komba na wengine wengi. Waamini na wageni waliofika katika hitimisho hilo waliweza kuingia kwenye birika la Betsaida lililokuwepo kwaajili ya watu kuacha shida zao zilizowatesa kuanzia Januari hadi Juni 2016. Baadhi ya watu walipokea nguvu za Mungu na wengine kutokwa na mapepo.
Kumbuka semina hii ilikuwa ni kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa kutulinda miezi sita tangia mwaka 2016 uanze, kuliombea Taifa la Tanzania, kumuomba Mungu atulinde na mabaya na kutufanikisha katika kazi zetu kwa miezi sita ijayo kumaliza mwaka 2016.