MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

NYOTA WA JOYOUS CELEBRATION WATIKISA KATIKA HUDUMA NCHINI UINGEREZA


Siku ya ijumaa na jumamosi iliyopita wapenzi wa muziki wa injili katika majiji ya Leicester na London nchini Uingereza wenye asili ya Afrika walipata wasaa mzuri wa kumsifu Mungu wkiongozwa na timu ya nyota waliowahi kuwa waimbaji na wapigaji wa kundi maarufu la muziki wa injili barani Afrika la Joyous Celebration la nchini Afrika ya kusini.

Waimbaji waliongoza mashabulizi hayo katika kumsifu Mungu na kumkandamiza shetani ni pamoja na aliyekuwa kiongozi wa muziki wa kundi hilo kijana Nqubeko Mbatha, Bheka Mthethwa na Siyabulela Satsha katika drum kwa upande wa waimbaji ni pamoja na aliyewahi kuwa mwalimu wa sauti wa Joyous mwanadada Ntokozo Mbambo wa Mbatha, Mahalia Buchanan, Duduzile Tsobane pamoja na mwanamama Zanele Mokheti almaarufu kama Zaza huku kijana Sibusiso Noah Mathembu akiwa ni mwimbaji pekee aliyebado ndani ya Joyous aliyeongozana na waimbaji hao wakongwe.

Waimbaji hao waliweza kukonga nyoyo za watu hususani wapenzi wa Joyous pale ambapo licha ya waimbaji hao kuimba nyimbo zao binafsi kutoka katika album zao bado kijana Sibusiso, Duduzile pamoja na Zaza waliweza kuwakumbusha wahudhuriaji nyimbo zao walizowahi kuwika nazo enzi wakiwa Joyous na Spirit of Praise kwa upande wake Zaza, huku Ntokozo aliimba nyimbo mpya katika album yake ya Spirit and Life pamoja na Filled lakini pia aliwakumbusha wapenzi hao wimbo uliompatia maarufu ndani ya Joyous uitwao 'In the shadow'. Wanamuziki hao wanatarajia kuondoka kurudi kwao wiki hii baada ya uwepo wao nchini Uingereza wa takribani wiki mbili


Kijana Sibusiso Mthembu alifungua sifa katika tamasha hili
Duduzile Tsobane akafuatia katika kumsifu Mungu
Ikaja zamu ya Mahalia Buchanan kumtukuza Mungu

Mwanamama Zanele Mokheti 'Zaza' akimsifu Mungu
Ntokozo jukwaani