RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

FUATILIA LIVE MKUTANO MKUU WA CUF HAPA

Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho.


Mwenyekiti wa mkutano mkuu, Julius Mtatiro akiendesha kikao hicho



Wanachama wa CUF wakiendelea na mkutano huo.

Chama cha wananchi CUF leo kinafanya mkutano wake mkuu katika ukumbi wa Blue Pearl, Ubungo Plaza ambapo hoja iliyopo sasa ni Taarifa kuhusu barua ya Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu uenyekiti wa CUF ambapo wajumbe wanajadili kuhusu kuitwa kwenye mkutano huo ili awepo wakati akijadiliwa au la.

Wengi wa wajumbe wametaka Profesa Lipumba aitwe wakati akijadiliwa huku baadhi yao wakisema haina haja ya kuwepo.

Mwenyekiti wa mkutano huo, Julius Mtatiro anasema viongozi wa mkutano huo hawana uwezo wa kusema Prof. Lipumba aitwe au la, maamuzi yote yapo mikononi mwa wajumbe wa mkutano mkuu.

Anaongeza kuwa, kwa kuwa barua ya taarifa kuhusu Profesa Lipumba kujiuzulu ilisomwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif, hivyo anamkaribisha Maalim ili aweze kuongea baada ya wajumbe kuchangia mada hiyo.

Maalim Seif anawaomba wajumbe kumsikiliza na anaeleza utaratibu wa chama na kuwa kama Profesa Lipumba angekuwa amesimamishwa na chama ingewezekana kuitwa mkutanoni hapo kusikiliza wakati akijadiliwa lakini Prof. Lipumba aliondoka mwenyewe na kama akiitwa anaitwa kwa utaratibu upi wakati aliamua mwenyewe?

Baadhi ya wajumbe wanasimama na kuanza kuimba Lipumba, Lipumba, Lipumba wakitaka awepo kwenye mkutano huo wakati akijadiliwa.

Wanachama wote, wapenzi, mashabiki na wananchi kwa ujumla wanaweza kufuatilia live mkutano huo unaoendelea muda huu popote pale walipo kupitia LINK HII: MKUTANO MKUU WA CUF