RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

KABLA HUJAMWOMBA MUNGU AKUPE KIATU, MSHUKURU KWANZA KWA KUKUPA MGUU WA KUVALIA HICHO KIATU.


Kuna baadhi ya maombi hauwezi kumwomba Mungu kama huna kitu fulani. Kwani kuna baadhi ya vitu ukiwa navyo ndivyo vinavyokuwezesha kuomba maombi hayo unayaomba. Kwani bila hicho kingine kuwepo, hata ukipata hicho unachoomba hauwezi kukitumia.

Inawezekana umemwomba Mungu akupe kiatu cha kuvaa lakini hadi leo hajakupa, lakini mshukuru Mungu kwa kukupa mguu wa kuvalia kiatu, kwani kama usingekuwa na huo mguu hilo ombi la kiatu lisingekuwepo. Kwani wapo watu wenye uwezo wa kununua viatu, lakini hawana miguu ya kuvalia viatu. Inawezekana unamwomba Mungu akumpe mtoto; lakini mshukuru kwanza Mungu kwa kukupa mume; au mke. Kwani ombi hilo la mtoto lisingekuwepo kwako kama usingekuwa na mume au mke. Kwani wapo wenye uwezo wa kutunga mimba na kutungisha mwanamke mimba lakini hawana waume au wake. Inawezekana uko kazini muda mrefu na haujapandishwa cheo; na umekuwa ukimwomba Mungu upandishwe cheo kazini kwako, lakini mshukuru Mungu kwa kazi uliyonayo. Kwani ombi la kupandishwa cheo lisingekuwepo kama Mungu asingekupa kazi. Inawezekana umemwomba Mungu akupe saa ya mkononi lakini hadi sasa hajakupa; badala ya kumlalamikia kwanini hajakupa saa mshukuru kwa kukupa mkono wa kuvalia saa, kwa sababu kama usingekuwa na huo mkono ombi la saa lisingekuwepo.

Ni kweli tunapitia changamoto, lakini wapo wenye changamoto kubwa zaidi yetu. Ukiona huna sababu ya kumshukuru Mungu, nenda hospitali ya rufaa iliyopo mkoa uliopo halafu zungukia wodi za majeruhi wa ajali, wodi za wagonjwa wa kansa, na wodi za wagojwa wa T.B utapata sababu ya kumshukuru Mungu.

Katika yote tunayopitia kama binadamu bado tunasababu lukuki za kumshuru Mungu. Mungu anajua changamoto unazopitia lakini anayo sababu nzuri ya kuiruhusu. Kwani chochote Mungu anachoruhusu kwenye maisha yetu huwa anasukumwa na upendo.

Maadamu bado tupo duniani, changamoto za maisha ni sehemu ya maisha yetu. Ndio maana Yesu akasema, “ULIMWENGUNI MNAYO DHIKI; LAKINI JIPENI MOYO; MIMI NIMEUSHINDA ULIMWENGU” (Yohana 16:33). Ni mbinguni tuu ndio tutapumzika milele. Ninapomsoma mtume Paulo huwa ninatiwa moyo. Paulo alipitia changamoto nyingi sana lakini hakukata tamaa. Katika 1Wakorintho 11:16-33 anaelezea changamoto alizopitia wakati anahubiri injili. Anasema kuwa amepitia magumu mengi katika kuihubiri injili anasema “KATIKA TAABU KUZIDI SANA; KATIKA VIFUNGO KUZIDI SANA; KATIKA MAPIGO KUPITA KIASI. Anasema kwa Wahayudi mara tano alipata mapigo arobaini kasoro moja. Mara tatu alipigwa kwa bakora; mara moja alipigwa kwa mawe(hapa alipigwa kwa mawe hadi watu wakadhani amekufa. Lakini waliompiga mawe walipoondoka aliinuka na majeraha yake na kwenda kuhubiri injili sehemu nyingine. Soma Matendo ya Mitume 14:19-20 ). Halafu magumu haya yote aliyopitia Paulo anayaita kuwa ni dhiki nyepesi anasema “MAANA DHIKI YETU NYEPESI, ILIYO YA MUDA WA KITAMBO TU, YATUFANYIA UTUKUFU WA MILELE UZIDIO KUWA MWINGI SANA (2Wakorintho 4:17) Kuvunjikiwa mtumbwi baharini, anaita dhiki nyepesi, kupigwa bakora, anaita ni dhiki nyepesi, kupigwa kwa mawe hadi karibu ya kufa anaita ni dhiki nyepesi. Daaah this MOG (Man of God) was so amazing !!

Unajua kinachotofautisha kati ya washindi na walioshindwa, sio changamoto wanazopitia, bali kile wanachofanya wanapopitia changamoto. Paulo alipopigwa mawe hakumlalamikia Mungu, bali alimshukuru Mungu na kuendelea kupiga kazi ya Mungu, kuna mwingine akianguka analala hapo hapo, kuna mwingine akianguka anakung’uta vumbi na kuendelea na safari. Kuna mwingine akipata hasara kwenye biashara anaamua kuacha biashara, kuna mwingine anatafuta mtaji tena na kuendelea na biashara. Kuna mwingine majibu ya maombi yanapochelewa anakimbilia kwa waganga wa kienyeji; kuna mwingine anasema nitang’ang’ana na Mungu kwenye maombi hadi kieleweke. Kuna mwingine anapopatwa na changamoto anamlilia na kumnung’ukia Mungu, kuna mwingine akipatwa na changamoto analia, akimaliza kulia anafuta machozi na kuingia kwenye maombi. FAILURE IS NOT FALLING DOWN BUT STAYING DOWN !! WHEN YOU FALL WAKE UP AND WALK AGAIN !!

Sikia nikuambie THE CHALLENGE YOU ARE GOING THROUGH CAN STOP YOU TEMPORARILY; BUT YOU CAN STOP YOURSELF PERMANENTLY!! Changamoto unazopitia zinaweza kukuzuia kwa muda, ila wewe unaweza kujizuia mwenyewe daima !! Kilichowazuia wana wa Israel wasiingie Kanaani sio shetani wala sio changamoto walizopitia bali ni wao wenyewe !! Kufeli kidato cha nne sio kufeli maisha, usikate tamaa eti kwa sababu umefeli kidato cha nne, simama na uanze upya; kama mumeo amekutelekeza na amekuachia watoto futa machozi na usonge mbele. Hauwezi jua hao watoto watakuja kiwa wakina nani baadae. Kamuulize mama yake Magufuli uone kama alijua kuwa mwanae atakuja kuwa Rais. Songa mbele no matter what !! Kuna mtu mmoja aliwahi kusema “KAMA HAUWEZI KWENDA MBELE KWA KUPAA BASI KIMBIA, KAMA HAUWEZI KUKIMBIA BASI TEMBEA, KAMA HAUWEZI KUTEMBEA BASI TAMBAA; FANYA KILA UWEZALO LILILO HALALI KUHAKIKISHA KUWA UNASONGA MBELE.

MAADAMU MUNGU YUKO UPANDE WAKO HAKUNA KITACHOKUSHINDA, SI SHETANI, SI MIZIMU YA KWENU, SI MALAIKA. Neno linasema Mungu akiwa upande wetu ni nani aliye juu yetu. Katika MAMBO YOTE TUNASHINDA NA ZAIDI YA KUSHINDA, KWA YEYE ALIYETUPENDA (Warumi 8:31,37).

NDIO MAANA NINASEMA; SISI NI ZAIDI YA WASHINDI !!

Mchungaji na Mwalimu Gibson Gondwe