RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

28.08.2016: MAELFU WAINGIA KATIKA KISIMA CHA BETSAIDA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 28.08.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" aliweza kuongoza maelfu katika kisima cha Betsaida. Watu waliweza kupitia katika maji hayo kwa lengo la kuyaacha matatizo yao katika kisima hicho. 

Kabla ya watu kuanza kuingia katika kisima cha Betsaida watumishi wa Mungu wakiongozwa na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare waliweza kufanya maombi kwa Mungu ili kila mtu atakayekanyaga katika kisima hicho aweza kuacha shida zake na kupata neema ya mafanikio katika maisha yao. 

Kisima hicho kimekuwa kikiweka mara kwa mara katika kanisa hili na watu wamekuwa wakishuhudia walivyoweza kupokea ,miujiza yao kama vile kupata kazi, kupata ada na kodi ya shule, uponyanyia, kuondolewa mikosi na laana, kuoa au kuolewa, kupata wachumba, kupandishwa vyeo, kuinuliwa, kupata kibali, kuheshimiwa n.k. 

Mungu ni mwema kwa walio wake na wale wenye imani ya kutosha. Bishop amekuwa akifundiasha watu kuwa na imani, kwahiyo kila jambo unalolifanya lazima uwe na imani kuwa litakuwa kama ulivyolipanga. Watu wengi sanawanakosa kuwa na imani na kuishi maisha ya kuypendeza Mungu, na ndio maana kila hjambo wanalolofanya kwa malengo ya kufanikiwa wanashindwa kwasababu hawaamini kile wanachofanya. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu baadhi ya waamini wa kanisa hili wamekuwa na imani katika lile wanalofanya na kutimiza yale wanayoagizwa na wachungaji wao kufanya. 

Kwahiyo watu wenye IMANI ndio wamekuwa wakifanikiwa hata wapitapo katika kisima cha Betsaida wamekuwa wakiamini kuwa mateso yao sasa basi, na hii imekuwa ikiwatokea katika maisha ya kawaida na kushangaa mateso yao yametweka na wamabaki kumtukuza Mungu

 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa wa kwanza kuingia katika kisima cha Betsaida