RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MARIDHIANO NI MUHIMU KUELEKEA SEPTEMBER 1 ASEMA ASKOFU GWAJIMA


Akizungumza wakati akihojiwa na kituo cha Television cha Star TV Askofu Dkt Josephat Gwajima amesema, "kuhusu mgogoro wa police na vyama vya siasa busara inahitajika, kwasababu vyama vya siasa vipo kisheria basi Jeshi la police lipate muda wa kuwasikiliza ili kulinda amani ya nchi maana hakuna kuhatarisha amani bila sababu"

Kuhusu kuenzi amani, amesema, " amani ni marighafi mama kwa uchumi na ukuaji wa hali ya nchi yoyote, hivyo kuitunza amani ni kitu cha muhimu kuliko vyote kwasababu bila amani hakuna kuhubiri injili, wala hakuna ujenzi wa uchumi"

Kuhusu mgogoro baina ya serikali na Upinzani, Askofu Dr Gwajima amesema, "ni muhimu yawepo mazungumzo, na kila pande zitoe hoja zake na kuleta Maridhiano badala ya kuishia kupigana ambapo madhara yake yataathiri watu wasiohusika