MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCH. FRANCIS MACHICHI ALIVYOWEZA KUWAOMBEA WATU WALIOFIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO SIKU YA JUMAPILI 14.08.2016


Mch. Francis Machichi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” siku ya Jumapili 14.08.2016 katika ibada ya kuangamiza ngome za shetani iliyofanyaika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwaombea waamini wa kanisa hilo na alikuwa na haya ya kusema, 
“Leo ni siku ya kuziangusha ngome za shetani, lazima ngome zianguke Paul anasema” wala hatembei kwa namna ya mwili bali tunazitumia zile silaha za Mungu. Ukipata muda soma 2Wakoritho 10:4-5, tunazitumia silaha katika ulimwengu wa roho ili kuziangusha ngome za shetani. 
Siku ya leo ni siku yako ya kuangusha ngome za shetani iliyokuzuia kuinuka, siku ya leo ni siku nzuri Bwana ameifanya ili ile ngome inayokuzuia lazima ikutoke ili kufikia mafanikio yako kwa maana Mungu anampango na sisi sema, “Nitafika kwenye muujiza wangu.” Pokea kama uaminiavyo kwa jina la Yesu Kristo.”
Baada ya maombi hayo aliweza kuwaombea wale wote waliokuja na karatasi walizoandika mahitaji yao kama walivyoagiza na Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.