RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCH. NOAH LUKUMAI ATOA UJUMBE MZITO SIKU YA JUMAPILI 07.08.2016 KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Hata kama kuna kazi umekosa hautaishia bila kazi lazima utakua na kazi, hata kama kuna pesa imepotea hauta ondoka bila pesa lazima pesa itarudi kwako. Maisha yetu ni Neno hatuwezi ishi bila Neno, hatuwezi kutembea bila Neno mwambie jirani yako” maisha yangu ni Neno la Bwana “ Unajua Neno la Bwana ndiyo pekee linaloweza kukutoa wakati umeshindwa kila kitu Neno la Mungu linaweza , Neno la Mungu linatosha. 
Maandiko yanasema utakula matunda ya kinywa chako kile unachokiongea ndicho kinacho tokea katika maisha yako. Mwambie jirani yako umenigusa kwa maana mimi ni mtoto wa Mungu. Mtu yeyote mbaya atayekugusa anatafuta moto umuunguze, anayekuchezea anatafuta Mungu ammalize yeyote anayekunyoshea kidole anaangalia anajipalia moto wa makaa juu yake.

Leo ni siku tumeibatiza na ni wiki ambayo tumetoka kwenye jangwa tunaelekea katika nchi yenye maji tele, tunakwenda kufanikiwa na kuwa watu maarufu duninia. Maneno yetu tunayotamka ya mafanikio yanakwenda kuleta uhalisia kwasababu tunamwamini Mungu atatimiza yale yatokayo katika vinywa vyetu. 
Sisi ni timu moja ambayo tunafanya kazi moja na ninashukuru kwa moyo wa ndani kwa kila mtu aliyeshiriki katika kipindi cha maombezi kilichokuwa kikifanyika wiki iliyopita. Na wewe uliyefunga na kuingia kwenye maombi kwa siku kadhaa, nataka nikuhakikishie kuwa maombi yako na kufunga si bure bali yatakua ni maombi Baraka katika maisha yako. 
Lazima Mungu aku-“promote” lazima Mungu akuinue maana Mungu yupo karibu na watu walio vunjika Moyo watu walionyenyeikea Mungu anakuwa karibu nao, kama unaamini sema, “Bwana Yesu ninapokea upako wa madhabahu haya ya Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Kwa wote waliofunga pokeeni upako huu, sema, “Ee Bwana Yesu ninajiunganisha na mafuta haya kwa jina la Yesu, Ee Bwana Yesu tawala maisha yangu kuanzia sasa hakuna kitakacho tuzuwia katika maisha yetu, sema, “ameni.” 


Endelea kuomba siku zote na kumkumbuka kumuweka mbele za Bwana Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwa ajili ya huduma kubwa ambayo Mungu ameiweka mbele yake. Bishop huyu anahuduma kubwa sana anahitaji maombi yako. 
Wewe ambaye umeamua kushikamana nae lazima uchukue upako iwe wa fedha, au wa huduma, au wa siasa, nasema, “Chukua upako mmojawapo au chukua upako wote”. Yawezekana unataka upako wa pesa, upako wa kujulikana, basi nyoosha mkono wako juu kwa Mungu na amini unapokea kutoka kwa Baba, na Mungu akupatie kwa Jina la Yesu Kristo. 

Katika maombi yako kumbuka sana kumuombea Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwani naye amekuwa akikuombea katika afya yako, biashara yako, mafanikio yako, mapito yako, na kila kitu ulichokuwa unakihitaji kupitia maombi yake. Ni zamu yako sasa ya kugeuza kibao na kuanza kumuombea

Ukisoma kitabu cha Isaya 42:5-9, kinasema, “ Mungu Bwana anena Yeye aliyeziumba mbingu na kuzitanda, Yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake , yeye awapaye pumnzi watu walio juu yake , yeye awapaye roho wao waendao ndani yake .Mimi Bwana nimekuita katika haki nami nitakushika mkono na kukulinda na kukutoa uwe agano la watu na nuru ya mataifa . 
Kuyafunua macho ya vipofu , kuwatoa gerezani waliofungwa , kuwatoa wale walioketi gizani katika nyumba ya kufungwa Mimi ni Bwana na ndilo jina langu na utukufu wangu sitampa mwingine wala sita wapa sanamu sifa zangu.Tazama mambo ya kwanza yamekuwa nami nayahubiri mambo mapya kabla hayajatokea nawapasheni habari zake. 
Leo nimeleta habari njema kwako utoke kwenye hili jangwa uende mahali ambapo Bwana ameshakuahidia. Jangwa ni mahali ambapo pamejaa kilio, pamekosa matumaini, kwa sababu hujui uendako maana bado upo jangwani hivyo unakumbuka sana vile ulivyovipoteza. Wapo watu wengi wamepoteza vingi lakini siku ya eeo vina kwenda kurudishwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazaleti. Amini na utaona muujiza wako.


USIVUNJIKE MOYO KWASABABU SAFARI YAKO HAITEGEMEI WANADAMU
Mungu akasema mimi ni Bwana niliyeziumba Mbingu na Nchi. Pia ni Yeye ambaye anawapa watu pumzi na uzima, amekuchagua wewe kwa kukushika mkono usipotee jangwani peke yako . Mungu amekushika ukiwa jangwani hutembei kwa akili zako yupo anayekushika mkono, hajakuacha Yeye ndiye aliyekutoa Misri bado anakupeleka mahali anapotaka. 
Bado upo njiani ukiwa kwenye safari ndefu ya kimaisha. Yawezekana kuna jambo linakusumbua lakini Mungu wako bado anakutetea na hilo jambo lako. Mahali ambapo hali inakua tete unashindwa kuelewa na ubaki kujiuliza, “Hivi ni nini ninacho kifanya mbona sielewi? Unaona kama vile Mungu hayupo kwa sababu ya jangwa unalopitia ambalo linasababisha mambo mengi kutofanikiwa na unakosa lile tumaini la ahadi ulizopewa na Mungu. 
Mwambie jirani yako, “Usivunjinge moyo na hatua ya kwanza ya kutoka jangwani.Usivunjike moyo kwa sababu safari yako haitokani na watu walio kuacha, safari yako haitokani na maisha ya nyuma, safari yako inatokana na Yule aliyekwambia toka nimekuahidia mahali pengine”. 

UNAPOKUTANA NA JAMBO MBELE YAKO UJUE KUNA NCHI YA AHADI
Na ukikutana na jambo lolote katika maisha yako ujue kuna Nchi ya ahadi mbele yako, ukikutana na mambo magumu mbele yako usidhani kwamba ndo umepotea hapana, wewe wakati unakutana na kitu kizito ndiyo wakati ambapo mkono wa Bwana umekaribia. Kuna usemi unasema, “Unapokaribia asubuhi giza linakuwa kubwa zaidi kuliko majira yote”. 
Kuna mtu ameingia mahali ambapo giza limeongezeka usiogope habari ya giza lililoogezeka, unatakiwa kujua kuna asubuhi inakuja mbele yako. Unaweza ukawa unapita ukajiuliza, “Mbona mambo haya yanakuwa mabaya?” Mambo yanapokuwa machungu zaidi ndio muujiza wako unapokuwa mkubwa. Ukiona mtu ambaye anaelekea mahali pazuri zaidi mara nyingi anakuwa na upinzani mkubwa zaidi, ukiona mtu anavita vikubwa ujue anaushindi mkubwa, ukiona anayesengenywa sana ujue maisha yake siyo ya kawaida, ukiona mtu anaye pigwa kila siku ujue yeye ni wa tofauti, ujue yeye siyo wa kuchezewa, ujue yeye kafikia hapo kwahiyo si wa kawaida.
 Mwambie jirani yako, “Nitakapofanikiwa kupita katikati ya jangwa (jaribu) ujue kuna mkono wa Mungu umenishika na kunivusha”. Na mara nyingi kilicho mbele yangu kama ni kibaya nguvu za Mungu hunivaa na kunishindia na mabaya. Vita vyako unavyopitia ni kwa sababu ya nguvu za Mungu zilizopo mbele yako, maisha yako ni kwa inatokana na jinsi ulivyoyapangilia, ukubwa wa huduma ni kwa sababu ya ukubwa wa kazi, wito ulio nao na ndio maana unapitia kwenye magumu, ndio maana watu wanakuacha ili mambo mazuri yaje mbele yako. 
 Usiogope kijana mchumba kakuacha ujue kuna mzuri anakuja zaidi ya huyo, na ujue Yesu hawezi kukutelekeza, ujue kuna mambo mazuri yanakuja zaidi ya pale. Mwambie jirani yako, “Vita vyako ndio ushindi wangu”, ukishamuona Goliati ujue Ikulu iko mbele yako, na ukishaona wewe kila siku mambo yako ni magumu ujue wewe unaenda kuwatawala wenzako, ukishaona utapitia kwenye moto ujue utapumzika, ukishaona watu wote hawapo upande wako ujue Jehova yuko upande wako. Kumbe ugumu wa maisha unapoishia ndio mwanzo wa heshima nyingine.


Kuna gari lipo kiwandani linatengenezwa kwa ajili yako, usiogope kwa kuwa huna nyumba kwani wapo watu wanasoma kwa ajili yako, wapo watu wanashughulika kwa ajili yako. Maandiko yanasema yale mambo ambayo watu hawajawahi kuona wala kusikia kwa masikio yao, wala hawajawahi kufikili kwenye fahamu zao, Mungu amewaandalia watakatifu Mungu amekuandalia nyumba. 
Unakaa kwenye nyumba mbovu lakini hautafia pale, unapita jangwani lakini unaishia kwenye ushindi. Sema mimi siyo mtu wa kawaida ndio maana napitia pagumu, unapopitia hali ngumu ujue wewe ni watofauti shinda hiyo Roho ya upweke