RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MCHUNGAJI ELIZABETH AFUNDISHA JUU YA KUSHIKAMANA NI CHANZO CHA UHAI WETU

Siku ya Jumapili 07.08.2016 Mch Elizabeth Lucas wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” aliweza kuf9undisha juu ya mshikamano ambao ni chanzo cha uhai wetu, alisema, “Mpende Bwana kwa moyo wako wote ili uwavute waliovunjika moyo ili waishi maisha ya wokovu, maisha ya kumcha Mungu. Unatakiwa kuwafanya watu wasimchukie Mungu ila waseme, “Mungu wa siku hizi ni mstarabu”. Jamani wokovu ni ulelule na haujawahi kubadilika, ni wewe kuachana na dhambi. Haitakus
aidia kitu kama unakuja kanisani na siku ya mwisho ukaenda motoni. Inawezekana ukawa unaimba sana, unawabariki watu sana, umefanya mambo ya kufanana na watu wa Mungu lakini huwezi kufika kwa Mungu kutokana na dhambi zako za chinichini.


Ninakuomba sasa anza kutengeneza maisha yako na Bwana ili uwe na msimamo wako wa kukusaidia kufika mbinguni. Nataka kukuambia kuwa uzima wa milele ni muhimu kwetu. Nimetumwa na Bwana leo kukuambia kuwa, “Tegeneza maisha yako na Bwana ile uwe na uzima wa milele”. 


Kuna watu wanasema, “mimi siwezi kuokoka na kuziacha starehe za dunia”, wanathubutu kumkana Kristo. Kuna watu wengine hata mavazi yao yanamdharirisha Kristo, hawavai mavazi ya kujistiri. Tunamuomba Kristo atusaidie kwa maana tunataka kuwavuta watu waje kwa Yesu na sio kuvutwa na shetani kutokana na mavazi yao mabaya wanayoyavaa na kumuudhi Kristo. 

Wakristo wenzangu, wokovu wetu ni wokovu wa ndani pamoja na nje kwahiyo tunatakiwa kuwa mfano kwa watu kwani sisi ni barua inayosomeka na watu wengi. Nakuomba sana usije kanisani nje mweupe na ndani ni mweusi. Kijana mmoja aliimba, “Wewe kanisani ni mweupi lakini kanisa ni mweusi”, ukirudi nyumbani mke wako unampiga mateke, unamdharau, unamnyanyasa, jamani nataka kuwaambia kuwa hatuendi mbinguni kwa jinsi hiyo.

Wakristo wenzangu tunatakiwa kutegeneza maisha yetu ili tuwe barua kwa watu na pia watu waweza kutamani maisha yetu, ili tuwe ni maji yaliyo hai na watu watamani kuyanywa. Ukiwa na Kristo hakuna kitu kitakachokutisha wala kukusumbua, hata kama unapitia magumu utasema, “Ninamjua anayenitetea na hili jaribu atanishindia, ninamjua mwenye ahadi zake”.

Kulia kwako sio bure, usitake watu wakuone unapomlilia Mungu wako, usijionyeshe kwa watu bali muangalie Mungu na kumlilia Mungu aliyekuokoka na atakayekuokoa katika pito unalopitia. Usitake kusifiwa na wachungaji, wainjilisti, washiroika au mtu yeyote bali tafuta kusifiwa na Mungu, kama alivyojisifia na kumwambia shetani, “Shetani umetoka wapi?” na shetani akasema, “Nimetoka duniani kuzungukua huko na huko”, Mungu akamwambia, “Umemuona mtumishi wangu Ayubu?”. Inatakiwa ifike mahali useme, “Jina la Bawana libarikiwe, kwani shetani anaweza kukushusha lakini Mungu anweza kukuinua na kukuwazia yaliyo mema”.

Ukitaka kuendelea kushikamana na Yesu endelea kusema, “Wewe Mungu ndio mlinzi wangu, wewe ndiye uzima wangu”. Ukisoma Zaburi 119:11, Biblia inasema, “neno langu nimeliweka ndani yangu ili lisije likakutenda dhambi bali likatengeneze maisha yako”. Neno la Mungu likikaa ndani yako linakufanya unakuwa imara. Ukisoma Zaburi 119:5, Biblia inasema, “Neno lako ni mwangaza wa njia zangu”, chochote unachofanya tanguliza Neno la Mungu. Ukitaka kumfahamu Mungu, tembea na Neno la Mungu ili likumulikie unapopita.  Mtu wa Mungu ninakupenda na Yesu anakupenda na Yesu anakupenda, siku ya leo ninakuomba ushikamane na Mungu wako, shikamana na Yesu na Yeye hatakuacha. Wanadamu wanaweza kukuacha lakini Yesu hatakuacha, Yesu haangalii sura ya mtu, Yesu ukimwambia nisamehe nay eye anakusamehe  na tena anavuta dhambi zako. Mwanandamu akikusamehe, kesho anakumbuka yale aliyokusamehe. Mungu anasema, “Anatupa dhambi zako mashariki na magharibi na hazitaungana tena. 



Ndugu yangu ni wakati wa kunyeyekea miguu pa Mungu. Huu ni wakati wa kupokea uzima wa milele kutoka kwa Mungu. Yesu ametununua, Yesu ametugharamia. Hata tunapoona sinema ya Yesu, tunaona jinsi walivyompiga na kumtesa kwaajili yako na kwaajili yangu. Kumbuka lile taji la miba alivikwa kichwani, kumbuka ule mkuki aliopigwa ubavuni ili mimi na wewe tupate uzima wa milele. Itakufaidia nini kupata mamia ya vitu hapa duniani na ukaukosa uzima wa milele.






Sasa nataka niombe na wewe, sema, “Ee Mungu Baba nimesikia Neno lako, kwamba nishikamane na wewe Yesu Kristo uliye chanzo cha uhai wangu, mimi ni tawi ndani yako, unanijua Bwana jinsi ninavyoenenda. Bwana wangu ni shahidi, pale nilipokukosea Bwana, ninatubu mbele zako kama mwanamke msamalia ambaye hakuficha dhambi zake, name dhambi zangu naziweka wazi mbele zako. Nisamehe Bwana usinihesabie hatia tena Bwana, nifutie hatia zangu zote, niwezeshe Bwana kuupata uzima wa milele. Amen”