MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTOTO MWENYE MIAKA 5 NICE KUHUBIRI JUMAPILI HII 28. 08.2016 MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Kwako wewe ambaye hujamjua bado na wewe ambaye unamjua Nice. Huyu ni mtoto wa maiaka 5 anayeishi jijini Arusha mwenye vipawa vikubwa ndani yake. Ni mtoto ambaye anauwezo mkubwa sana wa kujua maswala ya siasi, Biblia, mahesabu ya shule ya msingi na sekondari, lugha ya Kiingereza kwa kiwango cha juu sana. Mungu amempa neema hiyo tangia alivyokuwa mtoto mdogo sana, na alipofikisha miaka 3 aliweza kuhojiwa na kituo cha radio cha CLOUDS kilichopo Mikocheni “B” jijini Dar es Salaam kuhusiana na uwezo wake mkubwa wa kujua mahesabu makubwa. Mtoto huyu mpaka sasa hajaanza shule, bado yupo katika mikono ya wazazi wake.

Siku ya Jumapili 28.08.2016 ataweza kuhubiri katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa mama wa upendo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kuanzia saa 3 asubuhi na kuendelea. Pia ataweza kuonyesha uwezo wake aliokuwa nao na vipawa vyake alivyojaliwa na mwenyezi Mungu kama vile masuala ya siasa, Neno la Mungu, mahesabu makubwa ya shule za sekondari na shule za msingi.

Tunakuomba usikose ibada hii Jumapili Mlima wa Moto Mikocheni “B” kwa mama wa Upendo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare uone Mungu anavyowatumia watoto kuujenga ufalme wa Mungu, na pia utapata nafasi ya kujua malengo yake kwa sasa. Utaweza kumuona mzazi wake ambaye naye atasema neno kuhusiana na mwanae kuhusu kipawa na kipaji alichonacho cha kuwa na ufahamu mkubwa
 Nice ( kushoto) akifanyiwa mahojiano na mtangazaji wa Praise Power Radio 99.3 ( kulia ) siku ya Jumanne 23.08.2016

 Nice


 Nice
 Kutoka kulia ni Rulea Sanga wa Rumafrica, mzazi wa Nice, Stanley na Nice

 Kutoka kulia katibu wa Mlima wa Moto Mzee Kibona, mzazi wa NIce na Nice wakiongea baada ya mahojiano kumalizika