MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MZEE MALYA: ZINGATIA IMANI, UPENDO NA IWE NA MATUAMINI


Siku ya Jumapili 07.08.2016, Mzee wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B” Mzee Malya ambaye alikuwa ni muongoza ibada ya Jumapili alikuwa na haya ya kusema juu ya Upendo, Imani na Matuamini, alisema, “Katika imani ya Kristo tumefundishwa mambo matatu, kwanza suala la Imani (Faith), pili suala la Matumaini (Hope) na suala la Upendo (Love). Mungu wetu anatusihi kuchunga imani zetu na pia jinsi unavyojituma kutoa mbele za Mungu naye atakurudishia. Kama una imani na upendo Mungu wa Mlima wa Moto Mikocheni “B” atakurudishia mara mia kwa kile ulichotoa kwa kazi yake. Tuishi kwa imanai na matumaini kwasababu wote tunasafari moja ya kwenda mbinguni chini ya Askofu wetu Dr. Gertrude Rwakatare, msikilize yeye na nyenyekea mbele zake na ufalme wa mbinguni ni wako.

Unatakiwa kujua kuwa Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anayozungumza madhabahuni sio yake ila yeye anafanyika kama chombo cha kupitisha ujumbe wa Mungu kupitia kinywa chake. Ukimsikiliza na kufuata maneno yake utakwenda kufanikiwa katika maisha yako.

Mungu anasema usiogope kwasababu Mungu wa Mikocheni “B” yupo mahali hapa kukusaidia, kukuinua na atageuza maisha yako ya jana na kuwa mema, andaa siku yako ya kesho kupitia siku hii ya leo na usikate tama. Kama wewe ni mkulima na hukupata mavuno, usiogope kwani Mungu mwenye vyote bado yupo na ni mwaminifu, andaa shamba lako sasa ili kesho uweze kuvuna.”