MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

VIDEO: TUNACHAGUA KUMSIFU MUNGU NA WAFUNGWA WA JELA YA NAIVASHA

Tunatumai u mzima mdau wa Gospel Kitaa. kwa Jumapili ya leo ambayo inatufikisha karibu ya mwezi huu wa nane, tunakuletea chaguo kutoka jela yenye ulinzi mkali ya Naivasha.

Kama wewe hujapata sababu ya kumsifu Mungu, basi wenzako wameamua kumsifu Mungu kutokea huko waliko. Popote ulipo unaweza kulisifu Jina la Yesu kwa makubwa na magumu aliyokufanyia.

Mipango na Misri ndio nyimbo ambazo tunakuletea kutoka kwaya hii ya "Naivasha Maximum Security Prison Inmate SDA Choir".

Wimbo wa Mipango unaeleza namna ambavyo mpango wa Mungu ulivyo juu ya mwanadamu, kuanzia kuasi kwa shetani hata kuja kwa Yesu kuokoa wataoamini. Wimbo wa Misri unaeleza namna ambavyo wameteseka na dhambi Misri hadi Mungu akawaokoa na sasa wanaishi kwa raha Kaanani.
Tunatumai uimbaji huu wa wafungwa pamoja na walinzi wa huko gerezani utakugusa na kubadili kitu ndani yako kwa ajili ya utukufu wa Mungu.