RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

15.09.2016: TANZANIA TODAY NA CHANNEL TEN REPORT: MWENYEKITI BODI YA PAROLE TAIFA DR AGUSTINO MREMA AMEPENDEKEZA KUFANYIKA HARAMBEE MAALUM ITAKAYOSAIDIA WAFUNGWA


Mwenyekiti bodi ya Parole Taifa Dr. Agustino Mrema amependekeza kufanyika harambee maalum itakayosaidia wafungwa wa makosa mbalimbali ikiwemo kushindwa kulipa faini huku mwenyekiti wa kamati hiyo akiwa Mchungaji wa kanisa la Mlima wa Moto Dr Getrude Rwakatare.

Bwana Mrema ametoa pendekezo hilo jijini Dsm wakati akitoa shukrani zake kwa niaba ya serikali kwa Dr Getrude lwakatare kufuatia kuwalipia faini ya shilingi milioni 25 takribani wafungwa 78 na kufanikiwa kutolewa nje ambapo amesema kuwa itapunguza msongamano wa wafungwa magerezani na kuokoa fedha za serikali.

Amesema kuwa bodi hiyo inakabiliwa na uhaba wa fedha hali inayowalazimu watumishi ngazi mbalimbali za magereza kushindwa kutekeleza haki za wafungwa waliofikia muda wakutoka kifungoni hivo kupitia harambee maaalum ya “KUWAKOMBOA WAFUNGWA KUTOKA GEREZANI” wafungwa wengi watapata haki zao.

Kwa upande mchungaji Dr Geteude Lwakatare amesema huduma ya kuwasaidia wafungwa walioko magerezani inatarajiwa kufanyika kwenye magereza mengine ya nchi nzima.