RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE OGOPA RUSHWA FANYENI KAZI MTAHESHIMIWA NA MUNGU PAMOJA NA WANADAMU

Utakatifu ndio utatufanya tung’are, najua wapo watoto sugu hawajaanza leo walianza tangu zamani nao ni watoza ushuru. Mnashauriwa kutoa au kupokea rushwa na watoza ushuru, msichukue zaidi ya kiwango cha mtu bali mfanye kazi kama wafuasi wa Bwana, msimtishie mtu atoa ushuru kwa vitisho. Ukimtisha mtu atoe ushuru maana yake unataka akupe hela ya zaida. Biblia inasema, “Askari nao wakasema na sisi je tufanyaje?” Wakaambiwa, “Waridhike na mshahara wao”, mshahara wako kama ni mdogo lizika nao usitafute kumbambikiza mtu kesi ya uongo kwa sababu umepata nafasi ya “traffic police” nao wanasimamisha magari bila sababu, hiyo roho ya rushwa kwa maaskari nakemea ishindwe. Kila mtu aishi maisha kutokana na kazi yake na aridhike na kile Mungu amempa aishi maisha kulingana na hali ya uwezo wake asiishi “artificial life”. Wapo watu wanaishi ki - “artificial”, anajifanya anavyo kumbe hana, akikaa anasema, “Njoeni ofisini munione”. Ofisini siyo mtu kukaa bali ofisi ni ile inayoingiza fedha, kukaa kwako ofisini hakusaidii tunachoangalia ni kwamba ofisi inaingiza kiasi gani kwa siku au kwa mwezi? Sasa kama wewe umekuja kutapeli tunakwambia koma kabisa kwa jina la Yesu. Watu wanalia kwa sababu ya utapeli na mwingine amekuja hapa kanisani sio kusali bali kutapeli, anataka kufungia hurusi hapa kanisani na baadae ankukimbia, huu ni utapeli. Kama umekuja hapa kanisani kwa utapeli Mungu anakuona na yatakayo kupata usiniulize. 

Hivi ndivyo alivyosema Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 18.09.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”