RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION



BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE: USIJILINGANISHE NA WALIOKUZIDI, MUANGALIE MUNGU.


Katika kitabu cha 1Thimotheo 6: 6-10, Biblia inatufundisha ya kwamba, “Utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa, kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu, ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo”. Lakina hao watakaokuwa na mali huanguka katika majaribu na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha, ambayo wengine wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani na kujichoma kwa maumivu mengi. Tunaishi katika karne ya 21, tunaishi katika nyakati za mwisho wa dunia. Yesu yu karibu kurudi na mambo mengi yatatokea na moja wapo ni uasi, kukosa fedha, ukame nyumbani na mahangaiko mengi. Lakini sisi kama kanisa, kama watoto wa Mungu tunayo matumaini, Utakatifu pamoja na kuridhika na ulicho nacho. Tunafaida kubwa maana hautaangukia katika vitanzi vya wamataifa. Wengi wanapenda kujiringanisha na watu Mungu. Nasi tumejariwa hapa kanisani Mlima wa Moto Mikocheni “B” kukaa katikati ya waheshimiwa, matajiri, watu wenye makampuni, watu wenye uwezo wa aina mbalimbali. Lakini unapo ingia nyumbani mwa Bwana kama mtoto wa Mungu fuata kile kilichokuleta na sio kusumbua watu kwani hujui ametoka wapi? Hujui Mungu kamitoa wapi?, hujui maisha yake yapoje hadi amefika hapa alipo, amefanya nini? Ana miaka mingapi? Wewe unamiaka 30 unataka kulingana na mwenye miaka 70 inakuja kweli? “Uteuwa maana yake utakatifu, ucha Mungu na kuridhika. Ukiwa navyo hivi utafaidika sana na ndio utakao kufikisha mbinguni. Tafuta kwanza vilivyo juu ambako Mungu yupo. Lakini ukianza kusema, ”Mzee Malya anaendesha shangingi na mimi nataka kuendesha shangingi, utalipata wapi kama siyo kuiba? Mimi siwezi kulingana na Mtu ambaye yupo juu yangu hata siku moja ndio unakuta sasa wengine wanakuwa kaka poa kakuta lijimama anaendesha gari yuko bize anamfungulia geti ilimladi apate gari aendeshe anaishi maisha mepesi ya laisi hiyo roho ishindwe kwa jina la Yesu. Haya aliyasema Bishop Dr. Gertrude Rwakatare Jumapili 18.09.2016. Usikose Ibada Jumapili saa 3 asubuhi