RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HEADLINES KUTOKA VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII JUU YA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KUWATOA WAFUNGWA 12 KATI YA 78 WATAKAOTOLEWA MAGEREZANI

Mitandao na vyombo vya habari vimeweza kutoa habari kuhusiana na mama wa upendo Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kiongozi wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" alivyo weza kuwatoa wafungwa 12 kati ya wafungwa 78 wanaotakiwa kutolewa.

Zoezi hilo limefanyika jana 08.09.2016 katika Gereza la Keko na baadaye Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alielekea katika Gereza la Ukonga na Segerea kwa ajili ya kuendelea na shughuli hiyo.

“Waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto ndiyo waliochangia kiasi cha shilingi milioni 25 kwa ajili ya kuwatoa jumla ya wafungwa 78 katika awamu ya kwanza, na baadaye kanisa litaendelea na zoezi hilo.” Alisema Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Lengo kuu la kutoa msaada huo ni kuisadia serikali kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani ili waweze kurejea uraiani na kujenga taifa kwani kuendelea kuishi huko wanapoteza nguvu kazi ya kesho

“Hatutetei uhalifu, msaada huu siyo tu kupunguza wafungwa gerezani bali kurejesha nguvu kazi ya taifa na ndani ya familia kwani wazazi waliofungwa hapa ni masikitiko kwa familia na watoto wao, hivyo tumesaidia familia nyingi kurejesha amani na faraja kwao” Alisema Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Aidha Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amewaasa wale wote waliochiwa huru kutoka magerezani kuwa wananchi wema wanapoishi na kuacha kufanya vitendo vya uvunjifu wa amani na kujikita katika ujenzi wa taifa.

“Biblia inasema katika Mathayo 25:36 – 40 inasema kuhusiana na kuwaona walioko kifungoni, na mimi kama mtumishi wa Mungu nimeguswa kutimiza andiko hilo” amesema

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amewataka wanaoguswa na tukio hilo kujitokeza kwa wakati mwingine kuwasaidia wale waliofungwa kwa kukosa fedha za faini ili warudi tena uraiani na kushiriki katika shuguli za uzalishaji mali na maendeleo.
Baada ya kuwatoa wafungwa gerezani Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliongozana nao kanisani na kuwaongoza sala ya toba, aliwapa nguo mpya za kuvaa  na baadae aliweza kula nao chakula cha pamoja (pilau, soda na maji). Aliwaomba waanze maisha ya kumtegemea Mungu kwani yeye ndiye aliyeweza kuwatoa gerezani kupitia watumishi wake wa kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".  Pia waliweza kumshukuru Mungu kwa nyimbo. Bishop aliweza kutoa Neno la Mungu litakalo wasimamia katika maisha mapya ya uraiani. Haikuishia hapo pia aliwapa nauli kwa kila mmoja kiasi cha Tsh. 30,000 na kuwapeleka katika kituo cha mabasi cha Makumbusho.

Hizi ni baadhi ya links kutoka katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na zoezi zima la kuwatoa wafungwa gerezani ambao walifungwa kutokana na makosa madogo madogo na wakasomewa kifungo cha miaka zaidi ya miwili kwa kukosa faini ya kuweza kutoka gerezani.
BONYEZA HAPA: 
1. Global Publishers
2. Masaka Habari
3. Habari Katz
4. East Africa Television  ( EATV)
5. East Africa Radio (EAR)- Facebook
6. Muungwana Blog
7. Liwale Blog
8. Channel Ten
9. IPP Media