RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HIZI HAPA FAIDA MUHIMU ZA TENDE MWILINI MWAKO


 Tende ni tunda ambalo linaongoza kwa kuliwa sana katika kipindi cha mfungo ndiyo tunda pengine kuliko tunda lingine.

Pamoja na kutumika sana katika kipindi hiko pia lina ladha nzuri mdomoni, huku likisheheni madini na vitamini lukuki na hivyo kuwa na faida nyingi kiafya.

Miongoni mwa faida hizo ni kama hizi zifuatazo:

Ulaji wa tendo humsaidia sana mhusika kupata kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili.

Pia ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia.

Tende pia husaidia kuupatia nguvu mwili na kukuondoa uchovu, hii ni kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’.
Hali kadhalika tende ina madini aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini hayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.
Pamoja na hayo tende pia huwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa wa anemia, (kupungukiwa damu) wanapotumia tende huweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi.

Mbali na hayo inaelezwa kuwa matumizi ya mchanganyiko wa tende maalum yaani maziwa, asali na unga wa hiriki huweza kuwa msaada kwa wale wenye shida ya nguvu za kiume.

Tende vile vile huimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
Nachoweza kusema ni kwamba kuna faida nyingi za tende na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine.