RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

HONGERA RC MAKONDA


Mkuu wa Mkoa Dar es Saalam mh. Paul Makonda

Tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam mheshimiwa Paul Makonda amefanya mambo mengi na ambayo yanaonekana kwa uwazi. Mambo hayo ni haya yafuatayo:-

USAFI

Imekuwa ni kama desturi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi wakazi wa jiji la Dar es salaam na maeneo ya jirani kufanya usafi kufuatisha agizo la serikali kupitia kinywa cha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mheshimiwa Paul Makonda. Jamii mpya yenye mazoea ya kufanya usafi kila mwezi ilizaliwa desemba 09 mwaka jana, ni kufuatia mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli kuazimisha sherehe za uhuru kwa kufanya usafi na maazimo hayo ilikuwa ni kwa nchi nzima.

OMBAOMBA (MATONYA)

Ombaomba maarufu kama matonya jijini Dar es Salaam hapo awali maeneo ya Posta mpya na Kariakoo walikuwa ni wengi kiasi ambacho walikuwa wakisababisha kero kwa wakazi wengine walitumia muda wao kujitafutia riziki. Naweza kusema uteuzi wa kiongozi huyu ulikuwa sawia na anakitendea haki kiti chake cha ukuu wa mkoa. Omba omba bila shuruti wamekuwa wakitii amri ya kiongozi huyu, wengi wamerejea mikoani na wengine wamejikita katika kazi mbalimbali.

ULEVI NA ANASA

Kinywa cha mkuu wa mkoa kimepiga marufuku matumizi ya kilevi cha Shisha na uvutaji wa sigara sehemu za hadhara. Ni baada ya kuona athari za vilevi hivyo sambamba na kuwashawishi vijana kufanya kazi.

“Ndani ya mkoa wangu ni marufuku kuvuta sigara hadharani.” Muda wa kazi vijana wautumie katika kufanya kazi ili kuleta chachu ya maendeleo katika nchi yetu. Tumeshuhudia wakitiwa nguvuni vijana wanaofanya starehe ama wanaokutwa katika majumba ya starehe muda wa kazi. “Kuna Asasi za Kiraia (NGO) zinapokea misaada ili zitetee mashoga. Kwenye mkoa wangu hizo NGO zote nitazifuta” alisema mheshimiwa Paul Makonda.

BODA BODA

Mwisho wa juma hili viwanja vya Leaders Club manispaa ya Kinondoni walikusanyika vijana wa madereva wa pikipiki marufu kama Bodaboda, mkusanyiko huo ulipambwa kwa maandamano ambapo mkuu wa mkoa huyo, alitoa Rai kwa vijana hao yakwamba Bodaboda ni ajira hivyo waithamini kazi yao na kuthamini uhai wao kwa kufuata sharia za barabarani na kutumia vifaa kwa ajiri ya usalama wa dereva na abiria kipindi wanapokuwa barabarani.

MTI WANGU

Oktoba Mosi mwaka huu mheshimiwa Paul Makonda anatarajia kuzindua kampeni mpya inatakayoitwa MTI WANGU. Kampeni hii ni mahususi kwa kulinda mazingira kwa kuongeza idadi ya miti. Mji wowote wenye miti ya kutosha hewa huwa safi na mandhari ya kuvutia. Hivyo muheshimiwa anawaalika wanakazi wa jiji la Dar es Salaam katika kampeni hii ya MTI WANGU.