RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

JUMAPILI 11.09.2016: WATU WAZIDI KUBATIZWA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Siku ya Jumapili 11.09.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mch. Prisca aliweza kuwaongoza sala ya toba walioamua kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao. Wachungaji wa kanisa hilo waliweza kuwaombea pamoja na kanisa zima. Waokovu wapya waliongozwa kubatizwa kwa maji mengi baharini na baadae walirudi kanisani kwaajili ya kupata chakula na ratiba ya kuanza masomo ya kukulia wokovu.

Wakiwa bahari wakibatizwa kuna baadhi yao  walitokwa na mapepo na majini kutona na nguvu za Mungu zilizokuwepo mahali pale. Waokovu hawa waliweza kupokea Roho Mtakatifu na kujazwa nguvu za Mungu. Walionekana na furaha sana baada ya kubatizwa na baadae waliamua kuanza kumshukuru Mungu kwa nyimbo. 

Kama kanisa tunamshukuru sana Mungu kwa kuwapokea watoto wake ambao sasa wameamua kufuata njia zake za haki. Pia tunakushukuru wewe ulliyewaombea hawa ndugu zetu na sasa wanafurahia wokovu wao. Tuzidi kuwaombea kwa shetani ni muongo asije akwarudisha nyuma tena. Maombi yako ni ya muhimu sana kuokoa Roho za watu. Unapojiombea, kumbuka kuwaombea na hawa ndugu zetu ili siku ya mwisho tukamuone Mungu pamoja nao. Sio vyema kumuona ndugu yako anaingia motoni na wewe unaingi katika ufalme wa Mungu. Tujitahidi kuonyesha upendo na kujaliana.

Wewe ni balozi wa Mungu kwahiyo kila wakati tafakari cha kufanya juu ya hawa ndugu zetu. Kama unawafahamu jaribu kuwasiliana nao na kuwatia moyo wasonge mbele. Kumbuka kanisa ni wewe na sio mtu mwingine, na pia wewe umeumbwa kuwaokoa waliopotea. Yesu mwenyewe alijishusha kwaajili ya kuokoa roho za watu. 

Kuna watu wako mtaani kwako na unauwezo wa kuwaambia waje kanisani na wakaja, lakini umebaki ukiwaangalia na kuwacheka wakati wanateseka na nguvu za giza, Inapendeza sana kuona unapokuja kanisani unaoongoza na mtu mpya ambaye bado hajampokea Yesu Kristo ili aokoke. Utajisikiaje kuona aliykuwa anateseka na nguvu za giza akimtumikia Mungu na kufurahia ukuu wa Mungu?

Jitahidi kutumia mali zako na kipaji ulichonacho kwa kazi ya Mungu. Mungu hakukuumba kwaajili kumtumikia shetani au kuona mwezako anaingia kwenye njia mbaya bali alituumba ili tumtumike na kuokoa roho za watu. Mungu akusaidie ujumbe huu ukuguse na uanze kuufanyia kazi. Tunakushukuru sana wewe ambaye umetusaidia kuwapata hawa ndugu zetu walioamua kuokoa. Mungu akubariki sana.