MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MTANZANIA DR. UPENDO JBRIDE KUPATA TUZO YA HESHIMA PHILADELPHIA

Hakika Mungu anazidi kufanya mambo makubwa kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Dr. Upendo JBride. Mungu amemtoa mbali na anazidi kumpaisha mataifa hadi mataifa. Hivi sasa anategemea kupokea tuzo yake ya Heshima ya Shabach Gospel Music Awards kama "Inspiring Gospel Singer from Tanzania in America". Tuzo hizo zitafanyika 16/10/2016 nchini.

Taifa la Tanzania na Afrika nzima tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kupata mwimbaji huyu anayejituma kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji katika mataifa makubwa hapa dunia. Sio kila mtu ana neema hiyo, lakini Mungu ametupa jicho lake kwa Dr. Upendo JBride na amekuwa mwaminifu kwa kazi ya Bwana tangia akiwa mdogo mpaka sasa. Nyimbo zake zimekuwa na mguso na hisia kwa wale waliobahatika kusikia akiimba. Ni mwimbaji ambaye amejishusha mbele za Mungu na mbele za wanadamu. Hakika tunajivunia kuwa na mwimbaji huyu, tunachohitajika kufanya juu yake ni kumuombea na kumuunga mkono katika huduma yake kwa kununua albams zake, kumualika katika mikutano mbalimbali au makanisani ili azidi kumuinua Yesu Kristo kwa njia ya uimbaji.

Huu ni wakati wa kumtumikia Mungu kama watoto, vijana, wazee, vikongwe kwani hatuna muda mwingine wa kumtumikia Mungu kama huu. Ipo siku Mungu atatuita na kutuuliza mlifanya nini huko duniani kwaajili YANGU? Tumuige huyu dada ambaye mbali na kuwa na majaribu ya kidunia lakini amesimama IMARA na Bwana bila kuteteseka. Katika maombi yako jaribu kumuombea yeye na familia yake azidi kuimarikia na kuwavuta watu kwa Yesu kwa karama aliyopewa na Mungu.