MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

UNGANA NA BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE KATIKA MAOMBI HAYA

Mungu tunakushukuru kwa damu ya Yesu kristo iliyomwagika msalabani kwa ajili yetu. Baba tunashukuru kwa kujitoa kwa kristo kwa kututenga na maovu, tunakutukuza Mungu, tunakushukuru, tunaahidi Mungu kukutumikia na kuwa chombo kitakatifu. Mungu tunajikabidhi leo na tumejiandaa na mioyo yetu, tawala maisha yetu. Tunavunja kila tamaa za mwili zikatoweke kwa jina la Yesu. Iweni Watakatifu maana mimi Mtakatifu. Mungu tusaidie tusitende dhambi tena, Mungu tusaidie tusitende maovu tena, Mungu tusaidie tusirudie matapishi tena, Mungu tusaidie tufunike kwa damu ya Yesu. Asante kwa sababu Roho wa Mungu yupo ndani yetu aendelee kutenda mema.

Hivi ndivyo alivyokuombea mtumishi wa Mungu (Super Woman, Mtakatifu Mwenye Heri kama wadau wanavyomuita kwa sasa, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare siku ya Jumapili 18.09.2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Unakaribishwa ibada ya Jumapili saa 3 asubuhi