RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.10.2016: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE AZINDUA RASMI SHILOH TANZANIA 2016 SIKU YA JUMAPILI

Siku ya Jumapili 09.10. 2016 Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuzindua Shiloh Tanzania 2016 ambayo hufanyika mara moja tu kwa mwaka nchini Tanzania katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni “B”. alikuwa na haya ya kusema, “Bwana apewe sifa, leo tunazindua Shiloh Tanzania 2016 rasmi. 
Chukulia Shiloh hii kama harusi ya mtoto wako, au jamaa yako wa karibu amelazwa hospitalini, kwa hivyo ni lazima ushughulike ili jambo lako lifanikiwe, ile habari ya kutegeana tuiache. Mwenyekiti wa Shiloh hii ni mzee Martine Ulele na katibu wake Mr. Alex Mapanga. Sasa tusome Hagai 1:6, ”Mmepande mbegu nyingi mkavuna kidogo, mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji, mnajika nguo lakini hapana aonaye moto, na yeye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka-toboka. 
Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu, pandeni milima mkaletemiti, mkaijenge nyumba, nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana”. Sasa naomba tuombe, “Baba Mungu katika jina la Yesu nalibariki Neno hili likapenye likapate nafasi kwenye mioyo yao, wabariki Mungu wanapokwenda kutoa kwa utukufu wako Mungu nimeomba katika jina la Baba na Mwana na Roho nimeomba. Amen. 
Tuna mkutano mkubwa kongamano la mwaka ambalo linafanyika kila mwaka mwazoni mwa Desemba ni kusanyiko la watoto wa Mungu, ni kipindi kizuri cha kuondoa ukame katika maisha yetu ya kiroho, kumsikiliza Mungu anakwambia nini, kufunga mwaka na Bwana. Tunakuomba sana ushiriki kongamano hili ambalo litaanza tarehe 04/12 hadi 14/12/2016 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni ”B” DSM Tanzania 

Hakuna anayefanya kazi ya Mungu akapotea, kazi unayofanya ya kuamka saa11alfajiri wakati giza bado, majogoo yanawika, unakimbilia kazini lakini msharaha mdogo unaoupata na hata ukiupata ni kama umeutia kwenye kikapu chenye vitobo ukadongoka. Umekuwa unafanya kazi kwa kulalamika, unamanung’uniko, unasema pesa ndogo sana unayoipata, unajiuliza kodi ya nyumba unalipaje, maji unalipaje, nauli unalipaje, mchana ukienda kula hata soda unakunywaje?
 Lakini upo tu mwaka hadi mwaka, lakini leo umjaribu Mungu kwa mema ili aweze kukushika mkono wako, aweze kukutetea. Ni kilio chetu kuwa na wafanyakazi wenye raha, wanaofurahia kazi zao na wanalipwa mishahara mikubwa. Kupitia Shiloh Tanzania 2016 mchango wako wa kuiwezesha ikafanyika utabadilisha historia ya maisha yako. Katika Isaya Neno la Mungu linasema, ”Kuna atapanyae lakini huongezewa zaidi, kuna azuwiaye visivyo haki lakini huelekea katika kwenye uhitaji”, unapotoa unakuwa kama unatapanya, haujui hiyo hela utaiona lini? 
Lakini kumbe wewe ndiye mwenye hekima Mungu atakutetea, anasema uongezewe zaidi, utaongezewa utashanga mtu anakwambia chukua hii elfu 50, ikusaidia mtu mwingine chukua 100,000. Utaona watu wanakuhurumia bila sababu. Uko kwenye basi unashangaa mtu kakulipia, uko mahali pa mahangaiko unaona mtu anakwambia njoo hapa uchukue Tsh. 10,000. Hii ni sadaka yako inakuhurumia. Muhubiri 11:1 inasema, “Tupa chakula chako usoni pa maji maana utakiona baada ya siku nyingi”. Kwahiyo jitahidi Shiloh jitahidi utumike ili upokee.


 Mch. Francis Machichi (kulia)


 Mwenyekiti wa Shiloh Tanzania 2016 (kushoto) na katibu wake


 ¸