RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

09.10.2016: BISHOP DR. GERTUDE RWAKATARE NA WAUMINI WA KANISA WAFAGIA MATESO KWA IMANI, MCH. NOAH LUKUMAY AFANYA MAOMBI SIKU YA JUMAPILI

Mch. Noah Lukumay siku ya Jumapili 09.10.2016 katika ibada iliyokuwa imelenga kufagia kazi za shetani na maovu juu ya maisha yetu kwa imani ambapo watumini walileta mifagio ya kufagilia kwa imani, alisema, “Chochote kilichojinasia leo tunaenda kukifagia, ikiwa kunauovu mkononi mwako uweke mahali hapa wala usikubali uchafu kukaa pamoja nawe, usikupali upuuzi ukae hemaani mwako, kama kuna kitu chochote kibaya leo tunakifagia tunakitupilia mbali. Biblia inasema, ”Leteni mizigo”, kuna vitu ambavyo vinakushikilia, lazima vikae mbali na wewe, Yesu anakwenda kufanya mipango katika maisha yako utakapofagia tu na ule mfagio tuliokuomba uje nao, biashara yako inaenda kuanza kwa jina la Yesu. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare akiwa amevaa kitambaa kuziba vumbi wakati waumini wa kanisa hilo wakifagia pamoja na yeye

Mathayo12:43 inasema ”Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji akitafuta mahali pa kupumnzika asipate. Halafu husema nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka”, hata akija aona pako tupu kwakuwa tumefagia na kupambwa. Natamkia, “Neema yangu, moyo wangu, chochote kilichoingia ndani yangu, katika jina la Yesu, kila takataka zilizotupwa katika moyo wangu, leo nafagia kwa Jina la Yesu Kristo”. 
Haya matendo tunayoyafanya katika ulimwengu wa roho tunafanya pia. Kuna watu wameleta matatizo kwenye nyumba yako, wameleta shida kwenye moyo wako, lakini kwa ibada ya leo tunaamuru vumbi linyanyuke na liweze kumfuata huko aliko yoyote aliye kushikilia leo akuachie kwa jina la Yesu. Haya ni mambo ya kiroho, wale wanayoyajua mambo ya kiroho huwa wanafanya kwa kuyamanisha.


Kuna mtu anaweza akaja kwenye nyumba yako, akaweka gari juu yako ni zuri kumbe tayari ameshaharibu network yako ya mafanikio.. Mimi Mch. Noah Lukumay natokea umasaini, na kule nyumbani kwetu Umasaini, kuna mama mmoja alikuwa na ng’ombe ambaye amesha zaa alafu maziwa yanatoka lita ishirini (20), lakini akaja mtu mbaya akaangalia ile ng’ombe, na alipoingalia tuakashtuka “eeh!!”, mara yale maziwa yakakata kutoa lita 20, asubuhi yake mama anapambani kukamua maziwa anaona hamna kitu kinatoka, anabaki anashangaa, “Mbona maziwa hayatoki?” ng’ombe kajazia, akaanza kumpa chakula, maji na kila kitu lakini maziwa hayatoki, akajiuliza, “Ni kwa nini?” 
Kwa sababu kuna mtu alikuja na mamneno yake mabaya juu ya yule ng’ombe. Mama yule alipogundua akasema, “Mwanagu leo maziwa hayajatoka” Tukamuuliza, “Nani kaja?” Akasema, “Mtu fulani alipokuja, akashituka “eeh” aliposhituka tu maziwa hayakutoka tena”. Yule aliyekushikilia usifanikiwe na akavulugikiwe kwa jina la Yesu, sema..ameni. Tulipoomba tu mambo yakatiki. 
Sasa leo hii tukakamua maziwa kama kawaida kwako, yeyote aliyekuletea taarifa ili ufukuzwe kazini leo, tunamfukuza, tunamuondoa kwa jina la Yesu. Kuna watu wameshikilia nafsi yako labda kwenye ardhi yako au sehemu unazomiliki wewe bila kujua, na unaona mambo hayaendi. Anza sasa kujifungua kwa maombi ya vita juu ya adui yako. Funga na kuomba huku ukijitakaza mbele za Mungu. Acha maovu yako maana huko ndiko njia ya shetani anakopitia kuchukua nafsi yako. Tubu dhambi zako. 


Wakati Yesu amepelekewa mwanamke aliyezini akaambiwa, “Huyu anapaswa kuuwawa”. Yesu hakuchora juu bali alichora chini, unajua ni kwa nini? Kwasababu nafsi yake yule mama alifungwa kwenye ardhi. Yesu alipochora pale chini basi ardhi ile iliwahukumu. Walipokuwa wameshika mawe kumuua yule mwanamke, ikashindikana. 
Yesu akageuza kbao badala ya kumuua yule mwanamke ikawa ni yakumponya yule mwanamke. Aliyeleta habari ya kifo kwako leo tunamuondoa kwa jina la Yesu. Leo tumekuja na mifagio yetu hapa kanisani kama tulivyoagizwa na Bishop wetu Dr. Gertrude Rwakatare kuja nayo ili tunafagia ardhi kwa imani. 

Kama kuna mtu aliyekushikilia kwenye Ardhi leo akuachie katika jina la Yesu. Sema aniachie, wachawi walioshusha nazi ili wakukamate leo hawatakuona kwa jina la Yesu, yeyote aliyerusha mawe chini ili uanguke kwenye kazi yako leo amalizike kwa jina la Yesu. Nakueleza maneno ya ulimwengu wa roho ili ukayatambue. 
Mchawi au mbaya wako anapofagia anafagia huku anaongea maneno mabaya juu yako, na akiongea mabaya yanakukumba kama huna Mungu, hafagii akiwa amenyamaza. Lakini wewe ukiwa unafagia nyumba yako huku umenuna hauleti Baraka, wakati wengine wanafagia huku wanaimba achilia Baraka za Mungu, wakati unafagia hata hao waganga wanajua kuwa leo kuna moto unawaka, wakati unafagia kuna vitu vinajileta. Jitahidi kufanya mambo yako kwa imani yenye matendo. 


Mwambie jirani yako lazima ufunguliwe, yeyote aliyekuweka ardhini usifanikiwe, leo lazima utoke kwenye mnaso wa tope hilo kwa jina la Yesu. Bishop wetu Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kupata maono ya watu kuja na fagio kanisani ili waweze kufagia mateso yanayosumbua katika maisha yao. Kuna watu watafagia hapa kanisani kwa imani na wakienda nyumbani kwao mambo yanaanza kunyooka, wataitwa kazini kwa jina la Yesu, akili za watoto wao watainuka na kuafaulu shuleni, waume wao waliotoroka nyumbani watarudi,. Sema, “Leo ninafagia roho ya madeni iliyoletwa kwangu kwa jina la Yesu”. 
Nataka uelewe kwamba, Bishop Dr. Gertrude Rwakatare anachosema kina maana katika ulimwengu wa roho. Biblia inasema, “Musa akaambiwa, Haruni mwambie achukue udongo halafu auelekeze kwa wana wa Misri halafu aurushe angani nao udongo utakapo tua nje tu ya Misri majibu yataanza kutokea”. 
Kile kilikuwa ni kipimo katika ulimwengu wa Roho, kwahiyo hata wewe utafagia mateso yako kwa imani na yataondoka kwa jina la Yesu. Sema, “Chochote kilichorushwa kwenye anga na kikatua kwenye boma langu leo nakifagia kwa jina la Yesu Kristo. Chukua fagio yako na ananza kufagia ukisema, ”Nafagia magojwa, roho ya kukataliwa, roho ya kuonewa, kila aina ya mateso, kila kilichokusumbua leo tumekifagia kama vumbi linavyotimuka leo adui zako wakatimke kwa jina la Yesu. 


Yale magonjwa yaliyokung’ang’ania leo yameondoka kwa jina la Yesu kristo. Kuna mtu mwingine akipimwa anaonekana hana ugonjwa wakati yeye anaumwa kweli kweli na hajui ni kitu gani kinasababisha ugonjwa huo. Leo ugonjwa umetimuka kwa jina la Yesu. Na kila roho zinazotumwa hewani, zinazokuzuwia ili usifanikiwe tunazisambalatisha kwa jina la Yesu. Sasa naomba uchukue mfagio wako hapo ulipo na unyanyue juu, anza kutoa uchafu uliojuu eneo ulilolopo, fanya kwa imani huku ukitumia mfagio wako. 
Unapotoa uchafu huo, anza kujitamuikia mafaniko katika yale unayotaka Mungu akutendee. Pia ananza kukemea mabaya, mateso, maouvu uliyonayo ukisema, kwa kitendo hiki cha kutoa uchafu angani, naondoa kila tatizo juu yangu kwa jina la Yesu Kristo” Fanya kwa imani na sio kwa mazoea. Unajua tunavyofagia juu kuna mabuibui ambayo yanaleta mafua, yanaleta mapepo. Sema, “Kwa jina la Yesu, magonjwa ya homa, homa ya biashara, homa ya mahusiano, homa uya ndoa, homa ya vifo, humo ya kutengwa, homa ya kutopa kibali, homa ya kuonewa, homa ya kusengenywa na wakwe, homa ya kutozaa, homa ya kutooa au kuolewa na kila huoma ndani yangu, achia kwa jina la Yesu”. Leo ninaondoa wingu lililowekwa na majini, kila mnyama anayetumwa kwenye nyumba yangu, mapaka yanayolia usiku, leo naondoa, kila popo anayenyemelea nyumba yangu leo nafukuza kwa jina la Yesu. Sasa anza kuomba huku ukikemea mabaya.





\