MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

23.10.2013: MAMIA WAOKOKA SIKU YA JUMAPILI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Watu wengi sana waliweza kujitokeza katika madhabahu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 23.10.2016 kukabidhi maisha yao mikononi mwa Mungu. Watumishi wa Mungu waliweza kuwaombea na kuwaongoza sala ya Toba. 
Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na wachungaji mbalimbali walipita kwa kila mtu na kuwagusa na kuwaombea. Kupitia maombezi na nguvu za Mungu zilizotanda katika kanisa hili, watu wengi walitokwa na mapepo, majini na kila mitego wa shetani, na wakaanza kupiga kelele na wengine kudondoka chini wakilia kwa machozi mengi sana. 
Mch. Elizabeth Lucas

Hii inaonyesha ni jinsi gani watu wametekwa nafsi zao na wanaendeshwa kama remote katika maisha yao bila ya kujijua. Siku hii ililkuwa ni komesha kazi za shetani kwa waumini hawa wapya. Maombi yalifanyika kiasi kwamba hata shetani hakutamani tena kuweka hekalu lake katika miili ya hawa watu.

Mungu wetu hashindwi na kitu kama ukimpokea na kumfanya kiongozi wako kwa kila jambo unalwaza, unalofanya na unalofikiri kulianza kulifanya.

Baada ya maombezi na kuongozwa sala ya toba, watumishi hawa walipelekwa mahali maalum kwaajili ya UBATIZO WA MAJI MENGI na baada ya waliweza kufika kanisani na kupata vinywaji huku wakibadilishana mawazo na watumishi wa Mungu.

Sasa, ni zamu yako wewe ambaye unaona bado unao muda wa kuponda raha hapa dunia, na umekuwa hufikirii kabisa katika suala zima la kuokoka. Ninakushauri ukoka sasa kwani hujui litakalo kukumba hapoa baadae. 
Unaweza kuodoka nyumbani salama na ukaaga nyumbani kuwa unaenda sehemu fulani, mara njia unakumbana na kifo cha ajali au jambo lolote. Na ukumbi ulitoka nyumbani hata sala ya kutubu dhambi zako hukufanya. Sasa jiulize baada ya kif chako ni nani atakuwa mgeni wako huko mbinguni.

Ndugu yangu ninaomba jumapili hili ufike katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tukuongoze sala ya toba na kukuombea ili uweze kubatizwa na kumpokea Roho Mtakatifu atakayekuongoza kufanya yaliyo mema, atakuepusha na maadui zako, utafanikiwa katika maisha yako, utafikishwa kwa Baba mbinguni baada ya maisha ya hapa duniani.

Ibada yetu siku ya Jumapili inaanza saa 3 asubuhi hadi 8 mchana, na siku za katikatikati ya wiki ni kuanzia saa 9 mchana hadi usiku. Mungu akubariki sana...