RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

23.10.2016: PRAISE AND WORSHIP TEAM YA KANISA LA MLIMA WA MOTO YAZIDI KUBADILISHA MAISHA YA WATU KUPITIA UIMBAJI WAKE KILA ITWAPO JUMAPILI

Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa matendo makuu anayofanya katika kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B" lililopo jijini Dar es Salaam Tanzania kupitia watumishi wake aliowaweka kwaajili ya kumsifu yeye na kumwabudu.
Mzee wa kanisa Martha Komanya

Praise Team imekuwa ikifanya vizuri sana katika uimbaji wao na pia jinsi wanavyomchezea Mungu wao kwa moyo wote wa upendo. Kutokana na uimbaji wao, umesababisha upako kuingia kwa waumini wa Mlima wa Moto pamoja na wageni wanaofika kuabudu katika kanisa hilo.


Praise and Worship imefanyika baraka kea walio wengi. Kupitia uimbaji wao watu wengi wanapata faraja, wanaburudika, wanabarikiwa, wanafunguliwa, wanaponywa na magonjwa mbalimbali, na hii ni kutoka na nguvu za Mungu zilizomo katika nyimbo zao.

Kipindi cha uimbaji kikianza utaona kuna wingu fulani la uwepo wa Mungu linafunika kanisa, na mkono wa Mungu unaanza kutembea kwa kila mmoja mwenye uhitaji wa kutembelewa na Mungu.

Ni vyema na wewe ukaungana na ibada hizi za Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili saa 3 asubuhi hadi saa 8 na katikati ya wiki kuanzia saa 9 mchana hadi usiku.

Mungu anafanya yaliyo mema kwa watu wake kupitia watumishi wake hawa aliowachagua kwa kazi yake. Jitahidi Jumapili huu kuwahi ili upokee baraka zako. Ni vema kabisa kama utaongozana na watu zaidi ya wawili kuja kanisani ili nao waonye utamu wa Yesu kupitia Mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare ambaye ameteuliwa na Mungu kuokoa mioyo ya watu ili siku ya mwisho wakaonane na Mungu mbinguni. Mungu na akubariki sana.