RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

25.09.2016: SIKU YA JUMAPILI WENGI WALIFUNGULIWA BAADA KATIKA KIPINDI CHA MAOMBEZI

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" tunaamini na tunasimamia msimamo huu ya kuwa, "Ukimwamini Mungu na kutii yale aagizavyo katika kitabu chake Kitakatibu yaani Biblia, unaweza kupokea hitaji lako lolote kutoka kwake, kwasababu umeonyesha unyenyekevu KWAKE na kumheshimu"

Jumapili ya tar. 25.09.2016 katika kipindi cha maombezi ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B",  Mchungaji Kiongozi  Noah Lukumay aliongoza kipindi cha maombezi na uponyaji ambapo  Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliweza kuwatembelea waumini walipo na kuwaombea huku akiwagusa kwa mikono yake mahali wanaposumbuliwa. Baadhi ya waumini waliweza kupiga kelele kutokana na nguvu za Mungu zilizokuwa zikitoka kutoka kwa watumishi wake. Wengi wao waliweza kudondoka chini na wengine mapepo yalipiga kelele yakitaka kutoka kutokana na Moto wa Yesu uliokuwa ukiwaunguza.

Mungu anafanya mambo makubwa sana kupitia watumishi wake wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliojitoa kweli kufanya kazi yake. Kuna baadhi ya watu waliweza kushuhudia jinsi Mungu alivyowaponya na kuwaweka huru katika vifungo vya shetani baada ya maombezi kumalizika.

Inawezekana kabisa na wewe kuna jambo linakusumbua sana, na umekuwa ukifika kanisani kuombewa lakini bado unaona hupokei majibu yako. Unapoona wewe unaomba na huoni majibu unatakiwa kujiuliza ni sehemu gani huendi kama Mungu anavyotaka uende? Inawezekana kabisa ukawa umefanya yote mema lakini kumbe wewe bado unafanya mabaya kama umalaya, uongo, wizi, ulafi, tamaa, kutoheshimu wazazi wako, huheshimu siku ya Mungu na mengine kama hayo.
Mungu wa Mlima wa Moto anaonekana na watu wengi wanapokea mafanikio yao ya kimwili na kiroho kama vile walivyoomba. 

Tunakualika katika ibada ya Jumapili itakayoanza saaa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Jitahidi sana unapokuja, uje na rafiki au ndugu yako ili na yeye aonje utamu wa Yesu. Kama atakuwa na hitaji lolote, Bwana Yesu atashulikana naye na hatimaye atakuwa huru.

Kumbuka tupo duniani kwa kitambo tu, makao yetu yako mbinguni, ni makao ya kudumu, kwahiyo yaandae makao hayo ili na wewe siku ya mwisho ukafurahie ukuu wake.