MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

AGOMA KUSHUKA BAADA YA KUPANDA JUU YA MWEMBE


kikosi cha uokoaji kikiwa eneo la tukio.

…Zoezi la uokoaji likiendelea.

…Kijana akiwa juu ya mwembe.

MOROGORO: Kijana mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Vigogo, ametoa tukio la aina yake baada ya kupanda juu ya mti wa mwembe na kukataa kushuka kwa muda wa zaidi ya masaa manne.

Tukio hilo la aina yake limetokea katika kata ya Mwembesongo, Mkoani Morogoro na kukusanya watu wengi.
Kwa mujibu wa wenyeji wanaomfahamu walisema, hii siyo mara yake ya kwanza kufanya tukio hilo katika mti ule mkubwa maarufu mkoani Morogoro.

Wapo waliosema kwamba ni michezo yake mwenyewe huku wengine wakihusisha na imani za Kishirikina, kwa hiyo ule mti siyo mzuri kwani una mambo ya kishirikina. Mashuhuda hao waliongeza kusema kwamba Bwana Juma aliwahi kusema eti ipo siku atahakikisha ule mti anauangusha na kubakia kigogo tu kwani siyo mzuri hata kidogo huku akisema kwamba eti kuna vitu vimechimbiwa katika eneo lile ambavyo siyo vizuri.

Baada ya watu wa usalama kufika na kutaka kumshusha alikuwa akitembea juu ya mti akihama matawi na kuwafanya watu wa kitengo cha zima moto,Tanesco na Polisi kushindwa kumshusha. Hadi shuhuda wa tukio hili anaondoka eneo la tukio hilo saa mbili usiku alikuwa hajashushwa