RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. GERTRUDE ALIVYOWEZA KUWAOMBEA WATU WENYE TATIZO LA VIDONDA KWENYE MATITI NA SEHEMU MBALIMBALI SIKU YA JUMAPILI 25.09.2016

Mch. Noah Lukumay wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 25.09.2016 aliweza kuwaita watu wote wenye shida ya uvimbe katika matiti yao au kifuani. Na pia aliweza kuwaita wale wote wenye vidonda na matatzo mbalimbali wafanyiwe maombi. Watu wengi sana walijitokeza na wengine walionekana wakiwa wamshika picha za ndugu zao.

Bishop Dr. Gertrude Rwakatare na watumishi wa Mungu wa kanisa hili waliweza kuchukua nafasi zao na kuanza kufanya kazi ya Bwana ya kukemea na kuharibu kazi na mipango ya  shetani inayoharibu afya za watu na maendeleo ya watu. Watu wengi walionekana kuguswa na nguvu za Mungu zilizotawala hapo kanisani. Baadhi yao waliweza kuangushwa chini na wengine kupiga kelele wakihitaji kusaidiwa. Mungu aliweza kujidhihirisha kupitia watumishi wake.

Tuna kila sababu ya kumuinua Jehovah ambaye mtenda miujiza kwani  anaonekana katika kanisa lake la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kupitiwa watumishi wake ambao aliowaweka kwa kazi yake hapa duniani. Hakika kwa Mungu hakuna lisilowezekana, bali ukiamini.

Siku hiyo watu wenye mapepo, majini, vinyamkela na nguvu za kishetani waliweza kuangushwa na kupiga kelele, huku mapepo yakiomba kuondoka katika miili ya watu wa Mungu. Huyu ndiye Yesu tunayemhubiri Mlima wa Moto Mikocheni, anafanya maombo makuu na yanayoshangaza wamadamu.

Ninachotaka kusema ni kwamba, "Kuna nguvu katika maombi, ukiamini". Watu hawa waliamini kuwa wakifika katika madhabahu ya Mlima wa Moto watafunguliwa na kuachwa huru.
Sasa wewe ndugu yangu unayeteseka na huo ugonjwa wako, umehangaika kwa waganga na hujapata jibu, umezunguka huku na kule ukihitaji msaada lakini hukusaidiwa, tatizo lako limebaki palepale. Tunakukaribisha katika ibada ya Mlima wa Moto Mikocheni "B", kwani watu wengi wamefunguliwa na sasa wanafurahia wokovu wao na uponyaji walipokea kutoka kwa Yesu Kristo. Acha kusikiliza sauti za watu wanaokuzuia kuja kanisani kwa sababu mbalimbali. Unayeteseka ni wewe na sio wao, njoo kwa Yesu akuweke huru kama wenzako. Bwana anakuihitaji sana katika kazi yake, njoo akuponye.

Usafiri ni bure kabisa kutoka katika kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa hapa jijini Dar es Salaam. Utaona magari ya Mlima wa Moto au utasikia watu wakisema, "Kwa Mama" ingia humo na utafika salama. Ibada inaanza saa 3 asubuhi mpka saa 8 mchana. Mungu akubariki sana.