MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

HABARI PICHA ZA TAMASHA LA IT’S ON LA ANGEL BENARD LILIVYOFANA NDANI YA VCCT,DAR.Jumapili ya jana,Oktoba 9 katika kanisa la Victory Christian Center Tabarnacle mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Tanzania Angel Benard aliweka alama nyingine katika jiji la Dar kupitia tamasha lake la IT’S ON ambapo ni mwendelezo wa ziara zake za nchi nzima za kuwakusanya wana wa Mungu na kuabudu pamoja.

Katika tamasha hilo lililokuwa na mguso wa kipekee halikudhirihisha tu kipawa alichokirimiwa Angel Benard lakini kibali na mafuta ambayo Mungu ameweka ndani yake.Watu walijtokeza kwa wingi kumsifu na kumwabudu Mungu pamoja na Angel ambaye alisindikizwa na waimbaji wengi kama The rivers of Joy,Elly Joh,Paul Clement,Bomby Johnson,Robert,The Doxaz,Goodluck Gozbert na wengineo.

Tamasha hilo lililoanza mishale ya saa tisa lilifunguliwa na sifa na kuabudu kutoka kwa The Rivers of Joy kutoka VCCT na baadaye kuafatiwa na Gospel rapper Elly Joh kutoka Borne Kingz

Elly Joh akihudumu

Baadhi ya watu waliohudhuria tamasha hiloBaada ya Elly Joh,Robert naye akapanda madhabauni kuhudumu

Ikafika zamu ya The Doxaz kumwadhimisha Bwana..Baada ya The Doxaz,Mchungaji Sam akasimama kusema machache na kuomba pamoja na watu
Baada ya hapo,Bomby Johnson akapanda kuendeleza wingu la kusifu na kuabuduBomby akamwachia Kijiti Paul Clement..
Ukawadia muda wa kumpandisha Angel Benard kwenye stage.Mc Fred Msungu ndio ilikuwa kazi yake

Kwa staili ya aina yake Angel Benard na timu yake wakapanda na kubadilisha kabisa hali ya hewa


Outifits za Angel pia zilikuwa gumzo iwa wahudhuriaji


Angel ,uongozi wake na kamati ya maandalizi nao wakapata muda wa kutoa shukrani zao