MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MCHUNGAJI DAVID URIO. SOMO:BARAKA ZINAPATIKANA HEMANI MWA BWANA.


Zaburi 133:1-3 "Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza, Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Ni kama mafuta mazuri kichwani, Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni, Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake. Kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni. Maana ndiko Bwana alikoamuru baraka, Naam, uzima hata milele". Kupitia Efatha ndio mahali tunakopokea Baraka, ila katika kupokea hizo Baraka kuna mpinzani ambae ni ibilisi Shetani anatumia mwanadamu ili kuleta uharibifu na Mungu anatumia mwanadamu vilevile ili kupeleka habari zake, hivyo kwa Efatha anamtumia Mtume na Nabii J. E Mwingira ili kusababisha tufike kwenye Baraka zetu. Katika mazingira yeyote unayopitia iwe ni kazini au kwenye biashara yako zingatia Neno hili ndipo Bwana atatuma waviziao ili kukusaidia. 1wakoritho 16:9 "kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao".