RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MSAJILI WA MAHAKAMA KUU DAR AJITOA KESI YA BABU TALE


DAR ES SALAAM: Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Projest Kahyoza amejitoa katika kusikiliza shauri linalowakabili Wakurugenzi wa Kampuni ya Tiptop Connections ya jijini Dar es Salaam, Hamis Shaaban maarufu kwa jina la ‘Babu Tale’ na ndugu yake, Idd Shaaban.

Sheikh Hashim Mbonde (mwenye kanzu katikati).

Kahyoza alifikia uamuzi huo juzi, siku ambayo alipanga kutoa maelekezo maalumu kwa wadaiwa hao. Hata hivyo, mlalamikaji katika shauri hilo ambaye ni Sheikh Hashim Mbonde alimuomba ajitoe kwa madai kuwa hana imani naye.

Katika shauri hilo, Babu Tale na nduguye wanatakiwa kujieleza ni kwa nini wasifungwe jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama hiyo.

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilimtaka Babu Tale amlipe Shekh Hamis Mbonde, shilingi milioni 250 kwa kudaiwa kuvunja mkataba kati yake na Sheikh Mbonde wa kuuza na kusambaza nakala za mawaidha (DVDs) bila ridhaa ya sheikh huyo.