RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MWIMBAJI CHRISTINA MATAI ATOA SABABU ZA KUWA KIMYA KIMUZIKI,ZIFAHAMU HAPA..

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Injli Tanzania na Afrika Mashariki Christina Matai amezungumzia ukimya wake katika uimbaji ni kutokana na kumsikiliza Mungu na kujifunza Neno la Mungu na kuzipa muda Albamu zake za awali.

Akizungumza na GOSPOMEDIA, amesema kwamba ukimya kwa mwimbaji ni muhimu ili upate neno la kuimba kwa watu unaowahudumia”Kwenye ukimya kwa mwimbaji mzuri ni lazima utulie na ndio maana unakuta mwimbaji anarudia rudia nyimbo au melody kwasababu tu hawana muda wa kutulia na kuzipa nafasi nyimbo zao za awali ili ziendelee kupata nafasi kwa mashabiki sasa ukiwa unatoa toa kanda nyingi kwanza unawachanganya mashabiki zako unakuta sauti yako ya wimbo wako uliopita kwenye Albamu zinafanana tu, biti ni zile zile unabadilisha maneno tu sasa ndio nini jamani waimbaji mtulie ili muwe na utofauti kukaa kimya sio dhambi msitoe toe Albamu Asubuhi na jioni mpate na muda wa kujisomea neno”

“Ukitaka kujua waimbaji hawana muda wa kusikiliza neno wewe chukua muda wa kuhudhulia hiyo mikutano au Semina kubwa kubwa utaona wakimaliza kuimba wanapiga story na wengine wanaondoka kabisa jamani waimbaji tujifunze neno pia tukumbuke Huduma hii ya Uimbaji aliianza shetani kabla ya kufukuzwa Mbinguni unafikiri anafurahia kumsifu Mungu kuna gusa hivyo huduma yetu hii ina Vita sana jamani “Alisema Christina Matai.

Mwimbaji huyo aliyewahi kutamba miaka ya 2004 na Albamu yake ya YESU NI NANI, iliyokuwa imesheheni nyimbo nyingi kama TANZANIA na NAINGIA UWANJANI iliyompatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanzania na 2013 alitoa Albamu ya AKILI YAKO INAPOFIKA MWISHO HAPO NDIPO MUNGU HUANZIA, ambayo ndio ilikuwa ya Mwisho kuitoa na kwasasa amejipanga kiupya zaidi baada ya kukaa kimya takribani miaka mitatu yupo studio kwa maandalizi ya ujio wake mpya tena katika muziki wa Injili.

Mwimbaji huyu anajishughulisha zaidi na Ushereheshaji wa shughuli mbalimbali za kiserikali na za watu binafsi licha ya kuajiriwa na Serikalini katika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO,

Kwa mawasiliano na MC CHRISTINA MATAI kwa ajili ya huduma ya Uimabji na MC yupo tayari mtafute kupitia.

Simu/WhatsApp: +255754 376 620
Facebook: MC Christina Matai
Instagram: christinamatai
YouTube: Christina Matai