RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

SPIKA KATAJA VITU VITAKAVYOJADILIWA KWENYE BUNGE LINALOANZA LEO


 Nov 1 2016 tunatarajia kuanza kuzisikia headline za kutokea bungeni Dodoma ambapo vikao rasmi vya mkutano wa tano wa bunge la 11 utaanza.Jana Spika wa bunge Job Ndugai alikutana na waandishi wa habari Dodoma na kuelezea baadhi ya mikakati itakayofanyika ikiwa ni pamoja na kujadili muswada wa sheria ya za huduma za habari.

‘Mkutano wetu wa tano wa bunge la 11 unaanza  November 1 hadi November 11 2016 ambapo shughuli yake ya kwanza inaongozwa na kanuni ya 94 lengo likiwa ni kujadili na kupokea maoni kuhusiana na bajeti ijayo ya serikali‘ –Job Ndugai

‘Jambo lingine ni kwamba katika mjadala huo tunatarajia serikali itapokea ushauri kuhusiana na vyanzo vya mapato, vipaumbele vya uandaaji bajeti ijayo ambapo haya yote yatafanyika katika siku tatu mfululizo‘ –Job Ndugai

‘Kutakuwa na taarifa ya mkaguzi mkuu wa serikali yani CAG katika kazi zilizokaguliwa kwa mwaka 2014/2015 pia kutakuwa na majadiliano ya makubaliano ya makubaliano ya Afrika mashariki na Ulaya ambapo itaamuliwa sasa kama tuingie ama laa!‘ –Job Ndugai

‘Zaidi kutakuwa na miswada miwili ya serikali ikiwa ni pamoja na muswada wa sheria ya huduma za habari kwa mwaka 2016 pamoja na muswada wa sheria wa marekebisho ya sheria mbalimbali namba 3 ya mwaka 2016‘ –Job Ndugai