RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

VIDEO: MAMBO SITA ALIYOYAZUNGUMZA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUFIKA KENYA




Rais Magufuli leo October 31 2016 amewasili nchini Kenya kwa ajili ya ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo kabla ya Mkutano na waandishi wa habari leo October 31 2016 amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake. 

Rais Maguguli akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya, Rais Magufuli ametyazungumza mambo haya saba..

1.Rais Magufuli amesema watanzania na Wakenya ni ndugu kwa sababu watu wanafanya kazi pamoja, pia yapo makabila ambayo yanaingiliana kwa shughuli zao za kila siku na hata wanyamapori wanazunguka katika nchi zote mbili bila kujali mipaka

2. Rais Magufuli aidha amemueleza Rais Kenyatta kuhusu hali halisi ya Tanzania ya kuhakikisha Tanzania inakwenda mbele, akisisitiza kuwa anahitaji watanzania walipe kodi.

3.Rais Magufuli amemuhakikishia Rais Kenyatta kuwa Kenya ndio nchi ya kwanza kwa uwekezaji kuliko nchi zote za Afrika na amebainisha kuwa takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260 pia amesema kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044.

4.Rais Magufuli amewakaribisha wakenya wote wanotaka kufanya biashara hata kuanzia leo

5. Rais Magufuli amemshukuru Rais Magufuli kwa msaada alioutoa baada ya tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba 

6. Rais Magufuli amesema wameagiza Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili (Joint Commission Cooperation) wakutane kabla ya mwaka huu haujaisha.