RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

06.11.2016: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA ZA MLIMA WA MOTO SIKU YA JUMAPILI ZAKONGO MIOYO YA WATU KWA UIMBAJI WAO

Hakika Mungu amegawa vipawa na vipaji kwa kila mtu kwaajili ya kumtumikia YEYE, lakini wanadamu tumekuwa wagumu wa kutambua hilo na tumebaki tukitumia vipawa hivi na vipaji kwaajili ya kumuinua shetani.

Tuna kila sababu ya kusema asante Mungu kwa kutambua kile ambacho waimbaji wa kanisa la Mlima wa Moto Mikochheni "B" waliopo jijjini Dar es Salaam Tanzania ya kukutumikia wewe BWANA kwa moyo wao wote wakiwa bado vijana na wengine ni watu wazima na watoto.

Siku ya Jumapili 06.11.2016 tumeshuhudia uwepo wa Mungu ukitanda katika kanisa hili mara tu waimbaji hawa wa Joybringers na Happy Kwaya walipoanza kupaza sauti zao nyororo huku wakicheza kama malaika wa mbinguni wakimsifu na kumshangilia Bwana kwa vifijo na ndelemo kupitia uimbaji wao. Kwaya hizi mbili za Mlima wa Moto Mikocheni zimekuwa nguzo ya kanisa kutokana na mchango wao mkubwa sana katika kitengo cha uimbaji.

Kupitia uimbaji wao, watu wamekuwa wakiinua viwango vyao vya imani, wakifarijika, wakibarikiwa, wakiadibishwa, wakijifunza na kuelimishwa kupitia mashairi yao yenye mpangilio mzuri wakiongozwa Roho Mtakatifu.

Watu walio bahatika kuwasikia waimbaji hawa wataungana na mimi kwa hiki ninachokisema kwa Jina la Yesu, na kama hujawahi kuwasikia basi ninakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Ni masaa machache sana ambayo yatakusaidia wewe kujifunza kitu kupitia waimmbaji. Baada ya kusikia ujumbe wa Mungu kupitia uimbaji wao utaondoka ukiwa mtu wa tofauti sana ukilinganisha na ulivyoingia kanisani.

Unaweza kujiuliza utafikaje kanisani? Usafiri wetu ni bure kuanzia katika kituo cha Mabasi cha Makumbusho DSM, nje kidogo ya kituo utaona magari yetu ya Mlima wa Moto Mikocheni "B" au fika Mwenge kwenye mataa utaona watu wakisema " Kanisani kwa Mama Rwakatare", ingia humo na baada ya ibada utarudishwa kituoni. Mungu akubariki sana.