MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

06.11.2016 : WATU WAZIDI KUOKOKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI


Siku ya Jumapili 06.11.2016 kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kundi kubwa la watu waliweza kumpokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yao, pia waliongozwa sala ya toba na kuombewa na watumishi wa Mungu hatimaye  waliweza kubatizwa kwa maji mengi. Siku ya Jumanne walianza masomo ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kupitia mtumishi wake Bishop Dr. Gertrude Rwakatare kwani tuliona nguvu za Mungu zikitendeka katikati ya hao walioamua kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao kwa ishara na  miujiza iliyokuwa ikitokea wakati wakiombewa kwani wengi wao walitokwa  na mapepo, majini, na nguvu za giza.

Tunakukaribisha katika ibada za Mlima wa Moto Mikocheni "B". Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa utaona mabasi ya Mlima wa Moto MIkocheni "B" au utasikia watu wakisema "kwa mama " ibada zetu zinaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.