DANIEL AMIR SANGA AKIWA KATIKA BARBER SHOP YA HM MAFINGA AKIJIANDAA KWAAJILI YA HARUSI YAKE NA VERONICA ILIYOFANYIKA JUMAMOSI 19.11.2016 MAFINGA
Daniel Amir Sanga akiwa katika Barber Shop ya HM Mafinga akijiandaa kwaajili ya harusi yake iliyofanyika siku ya Jumamosi 19.11.2016. Daniel amemuoa Veronica. Ndoa ilifungwa katika kanisa la Lutherani Mafinga na sherehe ilianzia nyumbani kwa marehem baba yake Shoti-Amir Sanga na baadae kumalizikia katika ukumbi wa CF Mafinga. Harusi hii ilihudhuriwa na watu zaidi ya 600.
Barber Shop hii ni ya classmate yake ambaye amesoma naye Jitegemee Sekondari DSM. Wakiwa shuleni hapo, Daniel alikuwa mwenyekiti wa UKWATA na Bestman wake Huruma alikuwa katibu wa UKWATA. Walipomaliza masomo Daniel Sanga alirudi Mafinga na rafiki yake Huruma alibaki DSM kwani huko ndiko waliko wazazi wake. Katika kuhangaika na maisha Huruma aliamua kuja Mafinga kutafuta maisha, na ndipo alipoamua kufungua Barber Shop yake hii ya HM pamoja na ofisi yake ya secretarial. Cha kushangaza leo hii amesimamia harusi ya rafiki yake kipenzi Daniel Sanga na saloon yake imehusika katika kumkarabati.