RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUNGU NDIYE ANAYEJUA NJIA YA KUKUPITISHA KUELEKEA MAFANIKIO YAKO.


Kutoka 13:17-18a
"Ilikuwa hapo Farao alipokwisha kuwaacha watu hao waende zao, Mungu hakuwaongoza kwa njia ya nchi ya Wafilisti, ijapokuwa ilikuwa ni ya karibu; maana Mungu alisema, wasije wakaghairi watu hawa hapo watakapokutana na vita , na kurudi Misri; lakini Mungu akawazungusha hao watu kwa njia kwa njia ya bara kando ya bahari ya shamu;"

Wakati Mungu anawatoa wana wa Israeli kutoka utumwani kuelekea nchi ya ahadi (kanaani), mbele yao kulikuwa na njia mbili za kupita;
i)Njia ya nchi ya wafilisti
ii)Njia ya bara kando ya bahari ya shamu.

kama wana wa israeli wangepewa ruhusa njia ipi wapite kuelekea kanaani, bila shaka wangechagua njia ya nchi ya wafilisti kwa sababu njia hiyo ilikuwa ni fupi sana. 
Lakini Biblia inatuambia kwamba Mungu ALIWAZUNGUSHA watu hao, maana yake aliwapitisha njia ya mbali sana; njia yenye shida na taabu nyingi sana, lakini kusudi la Mungu lilibaki palepale ya kwamba lazima awafikishe kwenye mafanikio yao.

Hofu yake kuu ilikuwa WASIJE wakaghairi na kurudi nyuma (Misri) kwani sio mpango wake warudi utumwani, Mungu hakuangalia umbali wa njia bali aliangalia usalama wa njia ambao utapelekea mafanikio kwa watu wake.

Mtu yeyote alye OKOKA, anasafiri. Kuna safari za aina tatu (3) katika maisha ya Mkristo;
I) Safari kuelekea Mbinguni 
II) Safari kuelekea Mafanikio
III) Safari katika huduma (katika utumishi)

Tunajua kabisa ya kwamba Mungu siku zote anatuwazia mawazo ya Amani, si mabaya kabisa (YER 29:11), 
watu hujiuliza mbona pamoja tumeokoka, mambo bado si shwari kama tulivyofikiri, mbona kama hatutafika kwenye mafanikio!!??

kijana mmoja aliwahi kuniuliza, mbona kuna watu walikuwa wameokoka vizuri, pia walikuwa wanasoma sana tena kuliko mimi na mitihani ya ndani walikuwa wanafaulu vizuri tu; lakini matokeo yao katika mtihani wa mwisho yalikuwa mabaya sana; Je! Mungu alishindwa kuwasaidia wafaulu!!??

Najua wapo wengi wenye maswali kama haya katika maisha ya kila siku, ukizingatia Wakristo ni nuru ya ulimwengu;