MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MWIGULU AONYESHA MFANO KWA WADAIWA BODI YA MIKOPO, AANIKA MAREJESHO YA MKOPO WAKE


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameonyesha mfano bora kwa wadaiwa wa Mikopo ya Elimu ya Juu baada ya kuanika nyaraka za marejesho yake ya fedha alizokopeshwa na serikali kupitia akaunti yake ya Facebook na kuwataka Watanzania kurejesha mikopo kwa manufaa ya wengine.

Waziri Nchemba ametoa ujumbe huo ikiwa ni siku chache tangu Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kutoa siku 30 kwa wadaiwa sugu wa mikopo hiyo kurejesha mikopo yao.


Mhe. Mwigulu amewataka wadaiwa kulipa mikopo hiyo ili Watanzania wengine nao wapate fursa ya kusoma huku akisema kuwa amelipa deni lake kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2013.

Katika nyaraka hizo inaonyesha Waziri Nchemba alitumia muda wa miaka sita kulipa deni lake la Tshs 2,153,400 kwa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

Huu ndiyo ujumbe aliyouandika Mhe. Mwigulu kwenye akaunti yake ya Facebook;