MelK Premium Suits

TANGAZO MUHIMU

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BISHOP DR. M.E. ADMIN

BISHOP DR. M.E. ADMIN

SANDLANDS HOTEL KARIAKOO

MWIMBAJI SILVANUS MUMBA AITAKA SERIKALI ISIMAMIE SHERIA INAYODHIBITI WIZI WA KAZI ZA WAIMBAJI.


Mwimbaji na mwinjilisti Silvanus Mumba ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Nitasubiri ameitaka serikali kusimamia sheria inayodhibiti wizi wa kazi za wasanii ili wasanii waweze kufaidika na kazi zao.

Silvanus ambaye ameanza kujishughulisha rasmi na muziki wa Injili mwaka 2013 ameweka wazi kuwa watu wengi wanaonufaika na kazi za sanaa ni wale ambao hawajazitolea jasho.

“Natoa wito kwa Serikali, Wajitahidi sana kutengeneza Sheria ya udhibiti wa wizi za kazi ya Sanaa, na sheria hii iwe na Adhabu kali kwani hii inawapa fursa watu maharamia kufaidika kupitia jasho la wasanii” alisema Silvanus.

Kwa upande mwingine Silvanus ameweka wazi changamoto zingine anazozipata yeye na waimbaji wengine ambao ni wapya kwenye huduma ikiwemo ya kutopata ushirikiano kutoka kwa waimbaji wakubwa na ile ya kudharaulika kwa sababu tu hauna jina kubwa.
“Kwakweli sipendi sana hii tabia ya wasanii walio tangulia kukataa kushirikiana kufanya nyimbo na wasanii wapya, nina washauri watengeneze Forum itakayokuwa inawakutanisha kujadili mambo mbalimbali lakini pia kuweka mipango ya kufanikiwa mbeleni” alifunguka Mumba na kuongeza “Pia kitendo cha kudhalaulika, unakwenda kutoa huduma ya uimbaji kanisa Fulani, kwa mualiko rasmi, unaacha kila kitu kisha unakwenda pale wakakuhairishia ratiba, pasipo tarifa yoyote na hii imenitokea sio chini ya mara tatu nikahisi labda Muda wangu bado nisubiri kwa Mungu labda atanionesha tena na hii ndicho kilinisukuma niandike wimbo wa Nitasubiri“

Kama hujawahi kuitazama video mpya ya Silvanus Mumba “NITASUBIRI” unaweza kuitazama hapa chini.